WILAYA YA MAGHARIBI B UNGUJA.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatambua mchango mkubwa uliotolewa na Waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar katika kuijenga nchi.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Kilimo Umwagiliaji Maliasili na Mifugo Shamata Shaame Khamis katika hafla ya kumuombea Dua aliyekua Katibu wa Kwanza wa Chama cha Afro-shirazi Marehemu Sheikh Thabit Kombo huko Chukwani Wilaya ya Magharibi B.Unguja.
Amesema Serikali imeweka Utaratibu wa kisheria wa kuwaombea Dua waasisi hao waliotangulia ili kuwathamini na kuwaombea shufaa kwa mola kutokana na juhudi walizozifanya ya kuikomboa nchi na kuleta maendeleo.
Aidha Waziri shamata amesema dhamira kuu ya kuwaombea Dua Waasisi hao ni kuwaenzi na kukumbuka michango yao na kujifunza kuwa tayari kushiriki kuijenga nchi.
Akitoa Shukurani Mwanafamilia mjukuu wa Marehemu Muhidini Muhsin Ali amesema serikali inafanya jambo jema la kuwaombea Dua na kuwakumbuka Waasisi waliotangulia kwani wao ndio walioonyesha njia njema ya kuijenga na kuweka mshikamano na Umoja katika nchi.
Ameeleza kuwa umoja ndio nguzo muhimu katika nchi hivyo ni vyema kushikamana na kupendana katika kuijenga nchi na kuleta maendeleo zaidi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...