Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro ameahidi kupeleka timu maalum ya askari wa Jeshi hilo kwa ajili ya kufanya operesheni ya kuwakamata wahalifu wa pikipiki na hili kufanikisha ukamataji huo amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa sahihi za uhalifu kwa timu hiyo ya askari.

IGP Sirro amesema hayo akiwa Ngarenanyuki  wilayani Arumeru jijini Arusha ambapo pia amekemea vitendo vya uvunjaji vinavyotekelezwa na baadhi ya watu ikiwemo vijana huku akiwahamasisha wananchi kuanzisha vikundi vya ulinzi shirikishi kwenye maeneo yao.

Aidha, IGP Sirro ameonya tabia ya baadhi ya wananchi kujihusisha na kilimo cha bangi na kwamba Jeshi la Polisi nchini litaendelea kuwachukulia hatua kali za kisheria ikiwemo kuwafikisha mahakamani.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...