Viongozi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania ( TANAPA) wametakiwa kuongeza kasi ya maboresho ya huduma za kitalii katika maeneo wanayoyasimamia  ili kuendana na kasi na fursa zitokanazo na Filamu ya Royal Tour Tanzania.

Wito huo umetolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) alipokuwa akizungumza na uongozi na watumishi wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, Mkoani Iringa.

Licha ya kuupongeza uongozi wa hifadhi hiyo kwa hatua nzuri za maboresho ya huduma, Mhe. Chana amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameiheshimisha Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Filamu ya Royal Tour hivyo ni wajibu wa Kila mtumishi wa Wizara kuhakikisha anafanya kazi kwa mwendo wa heshima hiyo.

"Mhe. Rais mama yetu Samia Suluhu Hassan ametupa heshima kubwa  Wizara ya Maliasili na Utalii, sasa ni wajibu wetu kwenda na kasi yake katika utendaji wetu na kuongeza utayari wa kuendelea kupokea watalii wengi zaidi" Amesema Mhe. Chana

Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha Kamishna Msaidizi Mwandamizi Izumbe Msindai, ameleza kuwa baadhi ya Mafanikio ya Hifadhi hiyo ni pamoja na kuongezeka kwa watalii, Kuimarika kwa mahusiano mema kati ya Hifadhi na wananchi, kuongezeka kwa idadi ya  Tembo na kupungua kwa ujangili.

Waziri Chana yupo kwenye ziara ya kikazi kwenye Hifadhi ya Taifa ya Ruaha mkoani Iringa.










 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...