
Bi. Zainabu ambaye ni mkazi wa Buza, Dar es Salaam, amekuwa akisumbuliwa na
kansa kwa takribani miaka 2 tatizo ambalo linamfanya ashindwe kukaa au kusimama
na badala yake, amekuwa ni mtu wa kulala kwa muda wote asiyeweza kujisaidia kwa
chochote.
Katika kufanikisha jitihada za matibabu na kuguswa na hali aliyonayo Bi. Zainabu, Meridianbet kwa kushirikiana na Global Tv walifika nyumbani kwa mgonjwa huyu na kumpatia mkono wa pole ikiwa ni pamoja na mahitaji muhimu anayoyahitaji kwa sasa. Pia, Meridianbet imechangia kiasi cha fedha ambacho kitaongeza nguvu kwenye gharama za matibabu ambayo anayahitaji ili awezekurejea kwenye hali yake ya kawaida na kupona tatizo linalomsumbua.
Akizungumza baada ya kupokea msaada kutoka Meridianbet, Bi. Zainabu aliishukuru kampuni hiyo kwa kutumia muda na rasilimali zake ili
kufanikiwa kufika nyumbani kwake na kumsaidia kwa kidogo walichonacho. Pia, Bi. Zainabu aliitumia nafasi hiyo
kuiomba jamii nzima ya Watanzania kuweza kujitokeza na kumsaidia kwa chochote
watakachoweza ili awezekuendelea kupata matibabu ya kansa akiamini kuwa bado
ananafasi ya kurejea kwenye hali yake ya awali kabla ya kupata tatizo hili.
Kwa upande wa Meridianbet wakiwakilishwa na Bw. Amani Maeda ambaye ni Afisa Ustawi wa Jamii, alizungumzia kuguswa kwao na hali
ya Bi Zainabu ambaye walimuona kupitia kipindi cha Global Jamii na kama kampuni, waliona kuna kila sababu ya kuungana
nae na kumsaidia kwenye matibabu ambayo anayahitaji.
Huu ni muendelezo wa kampuni ya Meridianbet kuungana na jamii yote hasa kwa wenye mahitaji ili kurejesha
tumaini la maisha kwa waliopoteza matumaini kwa sababu mbalimbali.
Kama mwanajamii, Meridianbet
na familia ya Bi. Zainabu
Mohamed wanakualika
katika kuchangia huduma za matibabu na kujikimu katika mahitaji ya kila siku ya
Bi Zainabu ambaye yupo kitandani kwa miaka 2.
Unaweza kuwasilisha mchango au kuwasiliana na familia ya Bi Zainabu kupitia namba 0652837297.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...