
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imepanga kumsomea hoja za awali,(PH) aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Kijamii( CCK), Renatus Muabi(53) na mfanyabiashara ,Yusuph Yusuph Mei 19, 2022.
Hatua hiyo imefikiwa leo Aprili 28, 2020 baada ya upande wa mashtaka kueleza mahakamani hapo kuwa upelelezi wa kesi hiyo ya jinai namba 19/2022, umeishakamilika.
Washtakiwa Muabi na Yusuph, wakabaliwa na mashtaka mawili ya kujifanya ofisa Usalama wa Taifa( TISS) ambalo liko mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Rhoda Ngimilanga.
Mapema, wakili wa Serikali Mwandamizi, Mwanaamina Kombakono, ameieleza mahakama hiyo kuwa shauri hilo liliitwa leo kwa ajili ya kutajwa lakini upelelezi umeishakamilika na hivyo akaomba tarehe ya kumsomea mshtakiwa maelezo ya awali.
Kombakono baada ya kueleza hayo, Hakimu Ngimilanga aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 19, 2022
Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, inadaiwa Desemba 24, 2021 katika Benki Kuu ya Tanzania (BOT), iliyopo wilaya ya Ilala, mshtakiwa Muabi kwa nia ovu, alijitambulisha kwa Nguling'wa Balghe kuwa yeye ni Ofisa Usalama wa Taifa, wakati akijua si kweli.
Shtaka la pili, Julai 10, 2021 katika ofisi hizo za BOT washitakiwa wote wawili ,walijitambulisha kwa Clay Apio kuwa wao ni maofisa usalama wakati wakijua si kweli.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...