Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Tanga

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Tanzania Bara Abdulrhaman Kinana amesema Watanzania wanaendelea kumkumbuka Baba wa Taifa hili Mwalim Julius Nyerere kila siku waasababu enzi za uhai wake alijali utu wa kila mtu, uadilifu na moyo wa upendo dhidi ya wengine.

Kinana amesema hayo leo Aprili 25,2022 wilayani Korogwe mkoani Tanga alipokuwa akizungumza na Wanachama na viongozi wa wa CCM wa Mkoa huo ambapo pamoja na mambo mengine amewakumbusha kuwa mwaka huu Watanzania tunaadhimisha miaka 100 ya kuzaliwa kwa Baba wa Taifa.

“Baba wa Taifa hili Mwalim Julius Nyerere tangu amestaafu amefikisha karibia miaka 37 au miaka 40, Mwalimu kutokana na uadilifu wake kila siku yuko kwenye mioyo ya Watanzania, yuko kwenye midomo ya watu.

“Katika Bara la Afrika tuna nchi 54 lakini tujiulize kuna viongozi wangapi walioshiriki kupigania uhuru katika nchi hizo na sasa wanaheshima na kukumbukwa, fikiria katika Bara zima la Afrika nani anaheshima mpaka leo.Ni Mwalimu Nyerere tu ndio anatajwa kila siku wakati viongozi wengine wamesahaulika.

“Ukiangalia mambo ambayo Mwalimu Nyerere anazungumzwa nayo sio yanayoonekana kwa macho, ni ngumu kusema Mwalimu amejenga barabara hii au amejenga uwanja fulani, anakumbukwa kwa kujenga maisha ya watu, anakumbukwa kwa utu wake, anakumbuka kwa kuzikomboa nchi nyingine barani Afrika.

“Mwalimu Nyerere asilimamia haki, utu , ubinadamu, usawa, uhuru, heshima ya kila binadamu na hayo ndio anayokumbukwa nayo. Ndio maana tutaendelea kumthamini na kumeshimu, wakati wa uongozi wake aliheshimika na jamii za makundi mbalimbali na sababu kubwa ni utu na upendo mkubwa aliokuwa nao,”amesema Kinana.

Ameongeza ingekuwa Mwalimu Nyerere hakujenga misingi hiyo hakuna ambaye angekuwa akimkumbuka lakini alijenga misingi imara ya watu kuheshimiana , kuthaminiana na kupendana.

Hivyo amewakumbusha Wana CCM kuyaishi ya maisha ya Mwalimu Nyerere kwa vitendo, moja ni jambo kubwa alilosimamia ni uadilifu.“Tuzingatie udilifu , alikemea rushwa , alikemea wizi na ubadhirifu”.

Katika hatua nyingine, Makamu Mwenyekiti huyo wa CCM amewaambia wanachama wa Chama hicho kwamba wanaelekea katika mchakato wa uchaguzi wa ndani wa Chama, hivyo wazingatie kuchagua viongozi ambao watatokana na sifa za uongozi na si kuchagua viongozi kwasababu ya kutoa rushwa.

“Tuko kwenye mchakato wa kuelekea uchaguzi wa ndani ya Chama, kinachofanya CCM iheshimike na kuwa na nguvu ni uwepo wa haki ya mwanachama kuchagua na kuchaguliwa.Nichukue nafasi hii niwasihi wanaosimamia uchaguzi kuzingatia haki.“Tuache wanachama waamue wanayemtaka, wanachama wanawajua viongozi wao, wanajua nani wa kuwaongoza, nani anaweza kuwatutetea, kuwasemea.

“Hivyo tusikuabali kuchagua mtu ambaye anapatikana kwa kununua wapiga kura na kutoa rushwa, hiyo sifa ya ya Chama chetu.Niwasihi mzingatie uadilifu ili tupate viongozi wazuri wa kukitumikia Chama.Kuna watu wazuri wanaoweza kuongoza lakini wanaogopa kwasababu hawana fedha.

“Hivyo ni vema watu hao wakashawishiwa ili wagombee nafasi za uongozi, na wale wanaotaka uongozi kwa rushwa tuwakatae.Wapatikane viongozi ambao hatatokana na rushwa,”amesema Kinana.

Aidha amesema kuna baadhi ya watu wamekuwa na tabia ya kuwaambia wanachama kuwa wametumwa kugombea uongozi lakini wakiulizwa wametumwa na nani wanakosa majibu.






 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...