MAPOKEZI makubwa yamefanyika katika Mkoa wa Tanga baada ya kuwasili kwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Tanzania Bara Kanali Mstaafu Abdulrhaman Kinana.
Makamu Mwenyekiti huyo ambaye ameambatana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho Shaka Hamdu Shaka baada ya kuwasili katika mkoa huo amepata nafasi ya kuelezwa taarifa mbalimbali kuhusu Chama hicho.
Katika mkutano huo ambao umefanyika wilayani Korogwe wana CCM wa kada mbalimbali wamejitokeza kwa wingi wakiwemo wabunge wanaotoka katika Mkoa huo kumpokea na kumsikiliza Kinana .
Wakizungumza kwa nyakati tofauti viongozi wa CCM Mkoa wa Tanga wamesema pamoja na mafanikio utekelezaji wa Ilani ya Chama hicho unaendelea kutekelezwa ikiwa pamoja na kutatua changamoto za wananchi wa mkoa huo.
Kuhusu utekelezaji wa Ilani ya CCM,viongozi Mkoa wa Tanga wamesema utekelezaji unakwenda vizuri kutoka na usimamizi mzuri unaofanywa na Chama hicho.
Aidha CCM Mkoa wa Tanga wamemuahidi Makamu Mwenyekiti kwamba watahakikisha wanakuwa mkoa ambao hautakuwa tegemezi , hivyo wameweka mipango thabiti kuhakikisha unakuwa mkoa ambao unajitegemea kiuchumi.
Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga wamesema kwamba mkoa huo unampongeza kwa kuteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho na anastahili kupewa heshima hiyo kutokana na uzalendo wake uliotukuka kwa Taifa la Tanzania.
Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Tanga ambaye alipata nafasi ya kutoa salamu kwa niaba ya Mkuu wa mkoa huo Adam Malima, ..amesema kwamba wanaendelea kuchapaka kazi ili kuleta maendeleo.
Pamoja na mambo mengine amewasilisha taarifa ya Mkoa wa Tanga iliyokuwa inaelezea masuala mbalimbali huku akizungumzia mchakato wa Anuani za Makazi ambao umefanyika kwa mafanikio makubwa kwa kutambua mchakato huo wa anuani za makazi utakwenda kusaidia katika sense ya watu na makazi inayokwenda kufanyika Agosti mwaka huu.
Pia ametoa taarifa ya ujenzi wa makazi ya wananchi ambao wamehamishiwa Wilaya ya Handeni katika Mkoa wa Tanga wakitokea Hifadhi ya Ngorongoro na kwamba ujenzi wa makazi kwa ajili ya wananchi hao unakwenda vizuri na mkoa umetenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule.
Meza kuu ikishiriki shangwe kwa pamoja na Wanachama wa chama hicho katika ukumbi huo
Baadhi ya Bunge wa Majimbo ndani ya Mkoa Tanga,akiwemo Mhe Januari Makamba (Bumbuli),Mhe.Khamis Mwinjuma a.k.a Mwana FA na wengineo wakimlaki Makamu Menyekiti wa chama hicho Ndugu Kinana
Ni vifijo na nderemo ndani ya ukumbi
Ukumbi wa Lembeni mjini Korogwe umefurika wanachana na wafuasi wa CCM tayari kumlaki Makamu Mwenyekiti wao CCM-Bara ndugu Abdulrahman Kinana
Baadhi ya Wanachama wa CCM wakiwa nje ya ukumbi wakisikiliza hotuba ya Makamu Mwenyekiti CCM Tanzania Bara Ndugu Kinana
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Tanzania Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana akivalishwa Skafu mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Lembeni mjin Korogwe tayari kujitambulisha kwa Wana CCM,kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa Tanga Ndugu Henry Shekifu
Makamu Mwenyekiti Ndugu Kinana akitazama bidhaa mbalimbali zinazouzwa na mjasiliamali nje ya ukumbi
Makamu Mwenyekiti wa CCM Ndugu kinana akipokea zawadi ya kitabu chenye picha ya Mwenyekiti wa CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan
Ndugu Kinana akifurahia ngoma ya asili baada ya kuwasili nje ya ukumbi
MakamuMwenyekiti wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na baadhi ya Viongozi nje ya Ukumbi
Makamu Mwenyekiti akisalimiana na baadhi ya akina Mama wa CCM nje ya Ukumbi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...