Njombe
KAMANDA wa Polisi mkoa wa Njombe Hamis Issah amethibitisha kutokea kwa vifo vya watu 8 na 19 kujeruhiwa katika ajali ya gari aina ya Coaster T 287 CCY mali ya kanisa Katholiki Njombe iliyogongana na lori la makaa ya mawe.
Watu hao ni miongoni mwa Umoja wa vijana kanisa katoliki Jimbo la Njombe (UVIKANJO) ambao walikwenda kuwatembelea watoto yatima katika kituo cha Ibumila wilayani Njombe.
Ajali ilitokea jana majira ya jioni katika eneo la Igima wilayani Wanging'ombe Barabara kuu (TANROADS) kuelekea mkoa wa Ruvuma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...