Na Amiri Kilagalila,Njombe
Mwenge wa uhuru baada ya kuzinduliwa mkoani Njombe umekagua miradi 6 yenye thamani ya zaidi ya milioni 437 katika halmashauri ya mji wa Njombe na kukubaliwa na kukubaliwa na kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Ndugu.Sahili Nyanzabara Geraruma
Miongoni mwa miradi iliyokaguliwa mjini Njombe na kuzinduliwa ni pamoja na gari ya kuzolea taka aina ya tipa yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 157 kupitia mapato ya ndani ili kukabiliana na changamoto ya uchafu.
Mbele ya kiongozi wa mwenge wa Uhuru kitaifa,afisa mazingira wa halmashauri ya mji wa Njombe Nelson Mlwisa anasema hii ni kutokana na kuwapo kwa ongezeko la taka katika maeneo mbalimbali ya mji wa njombe.
“Lengo kuu ni kuimarisha usafi wa mji ili kudhibiti uwezekano wa kutokea magonjwa ya mlipuko na kuhakikisha halmashauri inaendelea kuongoza katika mashindano ya usafi wa mazingira kitaifa”alisema Nelson Mlwisa
Akijibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru likiwemo la namna wananchi wanavyo shiriki katika kuchangia utoaji taka hizo na hatua zinazochukuliwa kwa wanaokaidi kuchangia,mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Njombe Kuruthum Sadick amesema.
“Ambao hawawezi kulipa ushuru wa taka kuna sheria ndogo ndogo kwa hiyo kupitia sheria ndogo huwa wanawajibika kwasababu kwa mwezi ni 1000”alisema Kuruthum Sadick
Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa 2022 Ndugu. Sahili Geraruma amewataka wananchi kuhakikisha wanashiriki kikamilifu kuuweka mji katika hali ya usafi wakati wote.
“Wananchi hakikisheni mji wetu unakuwa safi,unaendelea kupendeza kwani gari la taka lipo na wewe kazi yako itakuwa ni kukusanya taka na kuweka mahali zinapotakiwa”alisema Sahili
Ela Sanga na Daud Mwihomeke ni wakazi wa Njombe , wanashukuru kwa kuongezeka kwa gari hilo ambalo sasa litaongeza kasi ya uondoshaji wa taka ngumu mjini njombe.
Mwenge wa uhuru 2022 umewashwa rasmi leo April 2 kitaifa katika uwanja wa sabasaba mjini Njombe na kuanza kukimbizwa kwa ukaguzi,uzinduaji wa miradi pamoja na kutoa ujumbe wake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...