Na Jane Edward, Arusha

Viongozi wa dini ya kiislamu 28 kati ya 61 waliokamatwa wakikabiliwa na mashtaka ya Ugaidi tangu mwaka 2014 ,wameachiliwa huru bila masharti katika gereza la Kisongo jijini Arusha.

Wakizungumza na waandishi wa habari jijini hapa Imamu Mohamed Said amesema wanaishukuru serikali ya Mama Samia kwa kusikia kilio chao na sasa wako huru na watuhumiwa 31 bado wako gerezani.

Amesema kwa miaka tisa waliyokaa gerezani upelelezi wa kesi yao ulikuwa haujakamilika katika kipindi hicho hali iliyofanya wao kupata madhila makubwa wakiwa gerezani ikiwemo wenzao wawili kufariki Dunia kutokana na sababu mbalimbali.

Vilevile amesema wanaishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuamua kuendelea kupunguza mlundikano katika magereza hapa nchini na kuiomba kuangalia urahisi wa kuendelea kutoa haki katika magereza hayo.

Akitoa ushauri kwa serikali amesema kuwa serikali pia itoe misamaha kwa wafungwa waliokaa gerezani kwa muda mrefu,wagonjwa na wazee ili kutoruhusu magonjwa ya milipuko.

Amesema katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadan waislamu na serikali kwa ujumla iwaangalie wafungwa katika mwezi huu katika chakula na wasipate changamoto ya futari kwa kuwa wapo wanaofunga katika mwezi huu .



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...