Na Jane Edward,Arusha
Wakulima wa shayiri nchini wamelalamikia changamoto ya ukosefu wa soko la uhakika wa zao hilo hali inayofanya wakulima kushindwa kuwekeza katika kilimo hicho kutokana na uhaba wa masoko hapa nchini.
Hayo yamebainishwa jijini Arusha na baadhi ya wakulima Waziri Madongo ,walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari na kutaka kilio chao kisikike kwa serikali.
Amesema kuwa wao kama wakulima wa shayiri hapa nchini Wana masoko mawili ambayo wanaya tegemea ambapo huuza shahiri kwaajili ya kutengenezea vilevi aina ya Bia Tanzania breweries pamoja na Serengeti breweries na kama sio wao basi hakuna soko kabisa.
Kwa upande wake Salome Munis ambaye ni mtafiti kutoka TARI seliani na mratibu wa zao la Shayiri Kitaifa amesema shayiri ni zao linalolimwa hapa nchini kwaajili ya kutengeneza Bia tofauti na ngano na kwamba zao hilo mbegu yake hununuliwa nje ya nchi hali inayofanya TARI seliani kuendelea kujielekeza kwenye tafiti ya zao hilo zaidi ili kutengeneza mbegu zitakazo patikana hapa nchini.
Ameongeza kuwa utafiti wanaofanya ni kupata mbegu bora ya shayiri itakayo endana na soko la sasa na kwamba soko la Shahiri ni kama limetupwa na halina soko lenye msimamo hali inayowapa wakulima changamoto ya kuendelea kujiwekeza kwenye zao hilo pendwa duniani.
"Mimi nimetembelea soko la Shahiri pamoja na watafiti wenzangu TBL pamoja na Serengeti ilikuzungumza kwa pamoja na kuona ni namna gani tutapanua wigo wa soko la uhakika na kupata mbegu za zao hilo hapa hapa bila kutumia gharama kubwa"Alisema Bi Salome
Aidha amesema kuwa kwa jitihada za TARI seliani wameshapata Tani 1379 ambapo mbegu hizo zitaongezewa thamani ili ziweze kuwa nyingi na wadau waweze kununua mbegu na kuweza kuzisambaza ili wakulima walime shahiri bora zilizofanyiwa tafiti kutoka TARI Seliani.
Salome anasema kuwa katika kukabiliana na changamoto hizo wao kama watafiti wanaona Tume ya Taifa ya Sayansi Teknolojia na Ubunifu (COSTECH) Ina wajibu wa kuendelea kuunga mkono jitihada hizo za zao la Shayiri ili kubaini mbegu bora za shahiri zilizofanyiwa Utafiti na kama nchi kupata mbegu zinazo toka hapa hapa nchini na sio kuagiza nje.
Vilevile amesema kuwa ombi lake kubwa kwa COSTECH pia ni kuona namna gani watatoa pesa kwaajili ya kuunga mkono jitihada hizo na kwamba zao hilo la shayiri halina wafadhili kutoka nje ya nchi mpaka sasa na hivyo Tume hiyo iangalie utafiti wa zao la Shayiri kwa macho mawili.
Shayiri ikiwa katika vifungashio tayari kwa kuuzwa.
Shayiri ikiwa shambani tayari Kwa mavuno.
Wakulima was zao la Shayiri wakiotesha zao Hilo Kwa kufuata mstari
Shayiri ikiwa juu ya gunia tayari kwaajili ya kupelekwa kupakiwa.
Shayiri ikiwa shambani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...