NA YEREMIAS NGERANGERA..NAMTUMBO.
Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa mwaka 2022 Sahil Nyanzabara Geramuma amezindua miradi 5 na kukagua miradi 4 wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma yenye jumla ya shilingi milioni 550.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge alizindua mradi wa ujenzi wa madarasa manne katika shule ya Sekondari Nanungu, alizindua zoezi la ugawaji wa vyandarua kwa akina mama wajawazito na wenye watoto wachanga,uzinduzi wa kiwanda cha kuchakata mazao na uzinduzi wa huduma za uwekaji anuani za makazi postikodi pamoja na nyumba ya kulala wageni katika kijiji cha Njalamatata.
Kazi zingine zilizofanywa na kiongozi huyo ni kukagua vibanda vya vikundi vinavyojihusisha na huduma ya utoaji elimu ya lishe kwa jamii,kukagua mradi wa uwezeshaji vijana wa mashine ya kukamulia mafuta ya alizeti katika kijiji cha Mwinuko,kukagua chanzo cha chemichemi ya maji kilichohifadhiwa katika kijiji cha Luegu pamoja na kukagua klabu ya wanafunzi ya kupinga rushwa katika shule ya sekondari Nasuli.
Akiongea wakati wa uzinduzi na ukaguzi huo kiongozi wa mbio za Mwenge alipongeza usimamizi wa miradi na kuwataka viongozi wa wilaya ya Namtumbo kuendelea kujitoa katika majukumu yao ili kusimamia miradi ya serikali .
Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Dkt Julius Kenneth Ningu pamoja na mambo mengine alimshukuru kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa kwa kuukimbiza mwenge wilayani Namtumbo salama na kumhaidi kutekeleza maagizo aliyoyatoa ya kuendelea kujituma katika kutekeleza majukumu ya serikali ya kusimimamia miradi yanafanyika kwa kiwango kikubwa. Mwenge wa uhuru kwa mwaka huu 2022 umebeba ujumbe usemao” Sensa ni Msingi wa mipango ya maendeleo “shiriki kuhesabiwa tuyafikie maendeleo ya taifa .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...