Na John Walter-Babati.


Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, mhe Pauline Philip Gekul ameipongeza timu ya soka ya Simba kwa kutinga robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kibabe kwa kuichapa bao 4-0 US Gendamerie mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.


Mhe Gekul akizungumza leo Jumatatu april 4 akifungua mashindano ya kusaka timu ya riadha ya mkoa wa Manyara katika kata ya Maisaka mjini Babati yaliyofanyika katika shule ya sekondari Kwang'.


Gekul amewataka mashabiki wa timu za Yanga na zingine kuungana kuishabikia Simba Sc kwa kuwa inapeperusha bendera ya Tanzania Kimataifa.
Amesema inapotokea timu inacheza kuliwakilisha taifa ni wakati wa kuweka ushabiki pembeni.


"Niwaambie kabisa wananchi mimi sina timu,wote ni wa kwangu,kwenye wizara tunalea michezo zaidi ya 78,wenzetu wa simba jana walikuwa wanajenga heshima ya nchi"alisema Gekul.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...