Raisa Said,Tanga

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Safia Jongo amepiga marufuku bodaboda kubeba watoto wa shule wadogo ili kuwakinga watoto hao na ajali za barabarani.

Akizungumza jijini Tanga, Kamanda huyo alisa kumekuwa na tabia ya wakazi wa Tanga kutumia bodaboda kama basi la shule kitu ambacho hakikubaliki kisheria.

Amesema kisheria mtoto wa chini ya umri wa miaka mitatu hadi tisa haruhusiwi kupanda pikipiki. “Lakini sasa sio mtoto mmoja tu wanapakiza zaidi ya mtoto mmoja, watatu hadi wanne,” amesema

Kamanda jongo amesema Polisi Tanga wameandaa mkakati wa kupeleka askari wa usalama barabarani katika shule zote ili watoto ambao wataletwa na pikipiki Maarufu bodaboda,, watoto watachukuliwa ili wazazi wakija watakamtwe Kisha wachukuliwe hatua za kisheria dhidi yao.

Alito wito kwa wakazi wa mkoa wa Tanga watii sheri bila shuruti na kuacha kutumia bodaboda kama usafiri wakati ambapo bodaboda pengine hawana sight mirror au hawana kofia za kinga (Helmet) au hata leseni na wanaendesha kwa mwendo hatarishi na kusababisha ajali barabarani.

" Ni marufuku watoto Kwanzia miaka mitatu mpaka tisa kubebwa kwenye bodaboda" amesema Kamanda Jongo

Naye mkazi wa jiji la Tanga, Elizabeth Kabage amesema wana wanatumia bodaboda kwa sababu ya uhakika wa usalama wa watoto.

“Sisi ambao hatuna magari au hatuna uwezo wa kulipia basi ya shule, suala hapa ni usalama wa watoto. Mtoto akipakia bodaboda una uhakika kuwa atafikishwa shuleni kwa sababu anapakizwa na mtu unayemfahamu na kurudishwa salama. Hakuna wasiwasi wa suala la kuvuka barabara,” amesema Kabage.

Imefahamika hapa kuwa sababu kubwa ya bodaboda kuchukua watoto wengi ni kutokana na kutaka kujipatia fedha nyingi kwa wakati mmoja.

Bodaboda mmoja wa Kange kasera ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema kuwa wakiwa wengi kila kichwa kimoja kinalipwa fedha hivyo akichukua wengi ana uhakika kupata fedha nyingi.

Naye Devotha Cassian, Mratibu wa Miradi wa Shirika lisilo la kiserikali la Northern Coalition foe Extractives and Environment (NCEE) alikubaliana na wazo la hali ya kiuchumi kusababisha wazazi kutumia bodaboda.

Hata hivyo amesema licha ya hali ya kiuchumi lakini pia ni hatari Kwa Usalama wa mtoto.

 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...