Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesema itaendelea kuboresha masuala mbalimbali ya kimichezo sambamba na kutoa hamasa kwa wachezaji.

NBC kama mdhamini wa Ligi Kuu Tanzania bara imetoa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Desemba Reliant Lusajo na kumpatia mfano wa hundi ya Shiling milion moja.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Mkuu wa Chapa na Mawasiliano David Raymond amesema NBC itaendeea kutoa hamasa kwa wachezaji na makocha kwa kil mwezi ili kukuza soko la ndani.

Amesema, katika kukuza soka la kiushindani kwa wachezaji wa ndani wamedhamiria kuboresha hali za wachezaji kwa kuwapatia zawadi za kila mwezi pamoja na kocha bora.

“Tumedhamiria kuboresha soko la ndani la wachezaji, na makocha kwa kuwapatia tuzo za kila mwezi ili kuhamasisha wafanye vizuri na kujitangaza kimataifa,”amesema Raymond

“Kwa leo tumekuja kutoa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Desemba Reliant Lusajo na tunarajia kutoa kwa Clatous Chama kwenye mechi ya Derby,”

Akielezea kuendelea kutoa hamasa kwa wachezaji, Raymond amesema huu ni mwanzo wataendelea kuboresha tuzo mbalimbali za wachezaji na kufika mbali.

Godwin Semunyu - Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano ya Umma akimkabidhi  mfano wa hundi ya Shiling milion moja mchezaji bora wa mwezi Desemba Reliant Lusajo
 Ndugu David Raymond- Mkuu wa Chapa na Mawasiliano akimkabithi Tuzo  mchezaji bora wa mwezi Desemba Reliant Lusajo
mchezaji bora wa mwezi Desemba Reliant Lusajo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...