Na.Khadija Seif, Michuzi TV

WAKAZI wa Jimbo la Mpendae Visiwani Zanzibar wamepata faraja Kwa familia ya Marehem Salim turkey Kwa kuendeleza yale mazuri kwa wananchi wake hususani kuwakumbuka watu wenye uhitaji katika kipindi cha Mfungo wa Ramadhani.

Akizungumza na Michuzi Tv Mtoto wa Marehem Salim turkey, ambae ni Mbunge wa jimbo hilo Toufiq Salim amesema mara Kwa mara wakati wa Mwezi wa Ramadhani Marehemu alikua akiwakumbuka watu wenye uhitaji na kugawana nao kidogo anachopata.

"Wananchi walijua hatutaweza kuendelea na utaratibu huo lakini kutokana na misingi mizuri aliyoacha mpendwa wetu, jukumu hilo tumelibeba sisi familia yake na Leo tumegawa Mkono wa futari Kwa takribani watu 4000 katika Jimbo la Mpendae hapa Visiwani Zanzibar."

Aidha Miongoni mwa vitu vilivyogaiwa Kwa watu hao ni pamoja na vyakula mbalimbali ikiwemo Mchele, Maharage,mafuta, Sukari,unga pamoja na pesa.

Mbunge wa Jimbo la Mpendae Toufiq Salim turkey akikabidhi baadhi ya Mahitaji Kwa Mmoja ya Wakazi wa jimbo hilo kama Muendelezo wa kumuenzi aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo hilo Marehem Salim turkey ambapo wakazi 4000 tayari wamepatiwa sadaka hiyo katika kipindi hiki cha Mfungo wa Ramadhani
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...