Na.Khadija Seif, Michuzi TV
MWANAMITINDO nchini Hamisa Mobetto ameingia Mkataba na Kampuni ya ubashiri (PM BET) nchini na amekua Balozi wa pili, wa kwanza akiwa Msanii Rayvan kutokea wasafi.
Akizungumza na Michuzi TV Mobetto amesema anashukuru uongozi wa Kampuni hiyo Kwa kumchagua na kuona ni mtu mwingine sahihi wa kuitangaza Kampuni na kushirikiana na balozi mwenza katika kuhakikisha wanafanya kazi zao.
"Nitashirikiana na Rayvan kuhakikisha tunaandaa wimbo na kazi nyingine ambazo Kampuni itahitaji tufanye Kwa ajili ya kuitangaza zaidi."
Hata hivyo Mobetto ametambulisha ramsi Kampeni ya "Shinda na Mobetto" ambayo italenga zaidi wanawake na kuhakikisha katika ubashiri wao wanashinda.
Pia Mobetto ameweka bayana kuwa anapendelea sana kuwa Mfanyabiashara na anafurahia zaidi kazi hiyo kuliko kuimba na kazi ya Mitindo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...