NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chamwino Mkoani Dodoma, Deo Ndejembi amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha upatikanaji wa Daraja katika Kijiji cha Chitaburi ambalo limegharimu kiasi cha Sh Milioni 97.

Ndejembi ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Membe iliyopo jimboni kwake ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kuzungumza na wananchi na kukagua miradi inayotekelezwa ndani ya jimbo hilo.

Ndejembi amesema ahadi yake kwa wananchi wa Kijiji cha Chitaburi kilichopo Kata ya Membe ilikua ni kuwapatia daraja kwani kwa muda mrefu nyakati za mvua wamekua wakipata tabu kuvuka korongo hilo jambo ambalo limekua kero yao ya muda mrefu lakini sasa imekwenda kuisha.

" Namshukuru sana Rais Samia kwa kutupatia kiasi cha Sh Milioni 97 kukamilisha ujenzi wa Daraja hili ambalo sasa linakwenda kuwa Muarobaini katika Kijiji chetu cha Chitaburi na Kata ya Membe kwa ujumla. Haya ni mapenzi makubwa yaliyooneshwa na Rais wetu na sote tunapaswa kumshukuru sana.

Mlinichagua kwa kishindo na nikaahidi nitatekeleza deni lenu kwangu la Daraja, leo nafurahi kufika hapa na kukatika juu ya daraja, lakini pia nimetimiza ahadi yangu kwenu ya Maji, Rais Samia ametupatia Sh Milioni 75 kwa ajili ya mradi mkubwa wa Maji ambao utahudumia vijiji viwili haya ni mafanikio makubwa sana kwetu," Amesema Ndejembi.

Amesema mafanikio yote ambayo yanaonekana katika Jimbo hilo la Chamwino siyo kwa nguvu zake pekee bali ni nguvu za Rais Samia ambaye amekua akiguswa moja kwa moja na changamoto ambazo zinawakabili wananchi wa Chamwino ambapo yeye pia ni mkazi wake.

Naibu Waziri Ndejembi pia amehamasisha wake kujitokeza kwa wingi kuhesabia wakati wa zoezi la Sensa za Watu na Makazi kwani kutaifanya Serikali itambue idadi ya wananchi wake waliopo Nchi nzima na kupanga vema mipango ya maendeleo kulingana na idadi ya watu wake.







 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...