Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) imetoa msaada wa mablanketi 150 kwa wazee Mwika mkoani Kilimanjaro ikiwa ni sehemu ya uwekezaji wake wa kuisaidia jamii. Msaada huo kwa wazee ulipokabidhiwa kwa niaba yao kwenda kwa Mwika Rotary Club.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo, Meneja wa kiwanda cha SBL Moshi, Alice Kilembe alisema kampuni hiyo inajivunia kutoa ushirikiano kwa Mwika Rotary katika kuwathamini na kuwahudumia wazee wanaoishi katika eneo hilo.

‘Mchango tunaoutoa leo kwa wazee ni ishara ya upendo na shukrani zetu kwa kazi nzuri waliyoifanyia taifa letu katika enzi za ujana wao." Jamii inapaswa kutunza kikundi hiki, na SBL inajivunia kuwa sehemu hii. Tunaamini mablanketi yatawalinda na baridi kali msimu utakapofika,' alisema.

Sambamba na mchango huo kwa Mwika Rotary Club, Alice alisema kuwa SBL imekuwa ikitekeleza programu kadhaa za kusaidia jamii ambazo hadi sasa zimenufaisha mamilioni ya watu nchini kote.

"Mnamo mwaka 2019, SBL tulianzisha mpango wa ufadhili wa masomo kwa ajili ya wanafunzi wanaosomea masomo ya kilimo katika vyuo vya ndani ili kuunga mkono jitihada za serikali za kupanua wigo wa wataalamu wa kilimo nchini, na hadi sasa zaidi ya 200 wamenufaika na mpango huu," alitolea mfano.

"Aidha tumejipanga na tunaendelea na programu nyingi za kusaidia jamii, kama vile kuhakikisha waishio vijijini wanapata maji safi na salama (programu maarufu ijulikanayo kama Water of Life). Hadi sasa tumetekeleza miradi 22 ya maji katika maeneo mbalimbali nchini tangu mwaka 2010, ambapo watu zaidi ya watu milioni mbili wamenufaika’, alikiri.

Programu nyingine alizozitaja meneja huyo wa kiwanda ni pamoja na kilimo biashara, ambacho huwasaidia wakulima wakubwa na wadogo kuongeza uzalishaji huku wakiwaandalia mazingira ya masoko kwa ajili ya mavuno yao.

Aliyekuwa Rais wa Mwika Rotary Club, Ester Towo, ambaye alimwakilisha rais wa sasa, Godrick Lyimo, aliishukuru SBL kwa msaada huo, akibainisha kuwa mchango huo ni chachu kubwa kwa shirika hilo, ambalo linategemea michango hiyo ili kuendelea kuihudumia jamii ya Mwika.

"Tunafurahishwa sana na mchango wa blanketi 150 kutoka kwa SBL kusaidia wazee wa Mwika na maeneo ya jirani hasa wakati huu wa mwaka ambapo baridi linakaribia. Mablanketi haya yatawawezesha wazee kupata joto la kutosha wakati wa msimu wa baridi kali hapa Mwika," anasema.

‘Wazee wengi wanaoishi majumbani mwao wanakosa msaada kwa sababu hawana mtu wa kuwahudumia. Hivyo basi, mchango huu ni mkubwa sana kwao ambao utawafanya wahisi kuthaminiwa na kutambuliwa kwa mara nyingine. Ahsante, SBL,' alimalizia.
Alice Kilembe, Meneja wa Kiwanda cha SBL Moshi (wa pili kulia) akimkabidhi mzee wa Mwika blanketi lake, likiwa ni miongoni mwa mablanketi 150 yaliyotolewa kama msaada na SBL kwa wazee hao kwenye viwanja vya mahakama ya mwanzo kata ya Mwika mkoani Kilimanjaro tarehe 9 Aprili 2022. Kulia ni Ester Towo, mjumbe wa kamati ya Mwika Rotary Club wanaoratibu huduma za wazee hao kata ya Mwika.
Alice Kilembe Meneja wa Kiwanda cha SBL Moshi (wa kwanza kulia) akiwakabidhi wajumbe wa Mwika Rotary Club moja ya mablanketi 150 yaliyotolewa na SBL kwenye viwanja vya mahakama ya Mwanzo Mwika tarehe 9 Aprili.


Alice Kilembe kwenye picha ya pamoja na uongozi wa Mwika Rotary Club na baadhi ya Wazee wa Mwika mara baada ya kupokea mablanketi 150 kwenye viwanja vya mahakama ya Mwanzo Mwika tarehe 9 Aprili.

Wafanyakazi wa SBL wakiwa kwenye picha ya pamoja na uongozi wa Mwika Rotary Club na baadhi ya wazee wa Mwika kwenye viwanja vya mahakama ya Mwanzo Mwika tarehe 9 Aprili.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...