KAMPUNI ya Smart Africa Group (SAG) imeendelea kuonyesha matendo mema katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani kwa watoto na waumini wengine kwa kuwaandalia futari jana Aprili 26,2022 Dar es Salaam.

Mapema wafanyakazi wa Kampuni hizo jana Aprili 26, 2022 asubuhi walianza kwa kutoa msaada wa vyakula kwenye shule ya kiislamu ya Mtambani kwa watoto yatima 50 wanaosomeshwa shuleni hapo.
Jioni kampuni hiyo iliandaa futari ya pamoja iliyowakusanya watoto yatima na waumini wa dini hiyo ikiwa ni sehemu ya kuwafariji.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi mtendaji ma muanzilishi wa SAG Edwin Bruno amesema kuwa kampuni hiyo imeguswa na maisha ya watoto hao wenye ndoto kubwa kwenye maisha yao na kwamba wameitumia siku hiyo kuwatia moyo kwenye masomo yao na kuona kana kwamba wazazi wao wapo.

Bruno amesema kuwa kampuni hizo zinajihusisha na teknolojia yenye kuunganisha watu hivyo wameamua kukutana na watu hususan wenye uhitaji kama mrejesho kwa jamii.

“Sisi tunajihusisha na Teknolojia ambayo inaunganisha watu leo tumeona tukutane na watu kuona wanamahitaji gani , mfano leo asubuhi tulikuwa Mtambani kwenda kuwasaidia watoto yatima ambao tumeona kuwa wamebeba ndoto kubwa kwa ajili ya taifa letu” alisema Bruno.

Bruno amesema kuwa kufanya hivyo nikurejesha shukrani kwa jamii kwa kuwa kampuni hizo zimepata tija na kupokelewa vizuri na watu.

Sheikh Adam Mwinyipingu Sheikh wa Wilaya ya Ilala amewapongeza na kuwaombea dua wafanyakazi wa kampuni hizo na kusema kuwa kwa kile walichokifanya watapata Baraka hapa duniani na akhera.

Sheikh Mwinyipingu amesema kuwa Mtume Muhammadi (S.A) ameshaeleza kuwa yule atakayemkarimu yatima atakuwa pamoja naye kwenye pepo ya daraja la juu kabisa huku akhera.

Wakati huo huo Sheikh Mwinyipingu ametoa nasaha kwa waislamu kuwa Ramadhani iwe funzo kwao waendeleze mema yaliyofanywa wakati wa ramadhani.

Sheikh Mwinyipingu ametoa taarifa kuwa sikukuu ya eid Elfitry inatarajiwa kufanyika Mei au 3 ambapo kitaifa itafanyika kwenye msikiti wa Bakwata.

Kwa upande wake, Warda Kimaro Mkuu wa Idara ya Chapa kutoka Vodacom ambao ni wadau wa na SAG amesema.. "Kwa siku kama ya leo tunafurahi kushirikiana na CAG kama wadau wetu nasi vodacom tunasema pamoja tunaweza"

Amesema SAG ni wadau wa mtandao huo kwenye masoko ambapo wanawaunga mkono kwa kufuturusha na kuwapa msaada wa vyakula watoto yatima.
Watoto wanaolelewa na msikiti wa Mtambani wakipata futari iliyoandaliwa na kampuni ya Smart Africa Group kwa wadau wao wa biashara na watoto hao, Dar es Salaam jana jioni.
Baadhi ya wageni waalikwa wakishiriki Futari iliyoandaliwa na Kampuni ya Smart Africa Group (SAG) kwa ajili ya wadau wao wa biashara na watoto yatima wanaolelewa katika Msikiti wa Mtambani, Dar es Salaam.
Ofisa Mtendaji wa Kampuni ya Smart Africa Group (SAG), Emmanuel Kawedi akizungumza jambo wakati wa futari iliyoandaliwa na kampuni hiyo kwa wadau wao wa biashara na watoto yatima wanaolelewa katika Msikiti wa Mtambani, Dar es Salaam.
Sheikh wa Wilaya ya Ilala, Adam Mwinyipingu aliyemwakilisha Mufti Mkuu Sheid Abubakar Zuber akizungumza wakati wa futari iliyoandaliwa na Kampuni ya Smart Africa Group (SAG) kwa wadau wao wa biashara na watoto yatima wanaolelewa katika Msikiti wa Mtambani, Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa Kampuni ya Smart Africa Group (SAG), Edwin Bruno (kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa futari waliyowaandalia wadau wao wa biashara na watoto yatima wanaolelewa katika Msikiti wa Mtambani, Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...