Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, ameshiriki mazishi ya Msanii Maunda Zoro, yaliyofanyika Toangoma, Kigamboni Dar es Salaam, (leo) Jumamosi 16 April 2022.

Katika mazishi hayo, Shaka alijumuika na wanafamilia na waombolezaji, ndugu jamaa na marafiki ambapo alipata nafasi ya kuwasilisha salamu za pole na mkono wa rambirambi kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan.

”Mhe Rais Samia yuko safari (ziara) amenituma nifikishe salamu zake za pole kwenu ndugu, familia, jamaa na marafiki sambamba na kuwasilisha mkono wa rambi rambi toka kwake, anatambua kuwa tasnia hii imepoteza msanii mahiri ambaye wakati wote wa uhai wake aliitumia Sanaa kufikisha ujumbe , kuburudisha, kuhamasisha na wakati mwingine kuiunganisha jamii kwa ujumbe, sambamba na kuenzi kipaji cha (babake) Mzee Zahiri Zoro lakini Maunda akiwa msanii anaechipukia alifanya vizuri sana” alisema Shaka katika sehemu ya maelezo yake.

Bwana Ametoa , Bwana ametwaa
Jina lake lihimidiwe
Apumzike kwa Amani Maunda Zoro.
Ameen.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...