Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
KLABU ya Simba ya Tanzania rasmi imepangwa kucheza na Klabu ya Orlando Pirates FC ya Afrika Kusini katika mchezo wa hatua ya Robo Fainali ya Michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF Confederation Cup) msimu wa 2021-2022.
Simba SC itaanza kucheza nyumbani kati ya Aprili 15-17, 2022 katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam wakati Aprili 22-24, Simba SC itasafiri nchini Afrika Kusini kumalizia nngwe yake ya mkondo wa pili ya hatua hiyo Robo Fainali.
Michezo mingine ni ‘derby’ ya Libya kati ya Al-Ittihad Club dhidi ya Ahli Tripoli, huku Pyramids FC ya Misri ikimenyana na TP Mazembe ya DR Congo na Al Masry ya Misri watapambana na RS Berkane ya Morocco.
Endapo Simba SC itafuzu Nusu Fainali ya Michuano hiyo itacheza na mshindi kati ya Al Ittihad na Ahli Tripoli, huku mshindi kati ya Pyramids FC dhidi ya TP Mazembe watacheza na Al Masry au RS Berkane.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...