Na PATRICIA KIMELEMETA

MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC), Dk. Germana Leyna amesema Madini joto ni moja ya kirutubisho muhimu kwa ukuaji mzuri wa mwili na akili Kwa Watoto walio chini ya miaka mitano.

Akizungumza hivi karibuni, Dk. Leyna amesema kuwa, endapo mtoto atakosa madini hayo, anaweza kupata madhara mbalimbali ikiwa ni pamoja na udumavu wa akili na mwili katika ukuaji wake.

" Ili mtoto aweze kuwa na afya bora anahitaji kula vyakula vyenye madini joto kwa ajili ya kukuza afya ya mwili na akili, hapo ataweza kuondokana na udumavu na kuwa mwenye Afya bora hata akiwa mkubwa," amesema Dk. Leyna.

Ameongeza kuwa katika kukabiliana tatizo la upungufu wa madini joto Taasisi hiyo inatekeleza programu ya kuzuia upungufu wa madini joto nchini kwa kutumia mkakati endelevu wa kuongeza madini joto kwenye chumvi (Universal Salt Iodation).

Amesema kuwa, mkakati huo unalenga kuhakikisha kuwa angalau asilimia 90% ya kaya zote nchini zinatumia chumvi yenye madini joto ya kutosha kama inavyopendekezwa na shirika la afya duniani (WHO).

Naye Daktari wa Watoto wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Mosses Karashan alisema kuwa, mtoto mwenye madini joto ana uwezo wa kutengeneza homoni aina ya 'Thyroxin' Kwa ajili ya kuimarisha afya ya mwili, ubongo, mifupa , nishati na Kumkinga na magonjwa mbalimbali tofauti na mtoto asiyekua na madini joto mwilini Ambaye yupo hatarini kupata tezi aina ya 'Thyroid'

" Mtoto mwenye umri chini ya Miaka mitano akiwa na upungufu wa madini joto mwilini, anaweza kupata tezi (thyroid) na kumsababishia kushindwa kukua ipasavyo, shingo inalegea, mwili hatungenezi nishati ya kutosha, ubongo wake unadumaa, jambo ambalo ni hatari," alisema Dk. Karashani.

Aliwashauri wazazi kuwalisha Watoto Wao vyakula vyenye madini joto Kwa ajili ya kuwajengea Afya ya mwili na akili Ili kuwapuesha na magonjwa ambayo yanaweza kuwarudisha nyuma katika ukuaji

Kwa upande wake,Mariam Juma ambaye ni mzazi anasema kuwa,Madaktari wamekuwa wakitoa elimu ya kuwalisha Watoto vyakula vyenye madini joto kwa ajili ya kuwajengea Afya ya mwili na akili.

" Kila tukienda kliniki wazazi tunahimizwa kuwalisha Watoto wetu vyakula vyenye mdini joto kwa ajili ya kuwajengea kiafya, jambo ambalo limesaidia kupunguza magonjwa mbalimbali yakiwamo ya udumavu," alisema mariam.

Aliwataka wazazi kuzingatia elimu inayotolewa na watalaam wa afya wawapo hospitalini Ili waweze kuwakinga Watoto Wao na magonjwa mbalimbali.

Serikali ilizindua Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto(PJT_MMMAM) ambayo imelenga kujibu changamoto za mahitaji kwa watoto wadogo ambayo wanakadiriwa kufikia milioni 250 wenye umri chini ya miaka mitano wanaopatikana kwenye nchi zenye uchumi wa chini na kati ambao wapo kwenye hatari ya kutofikia hatua za ukuaji,

Kwa upande wa Tanzania, asilimia 43 ya watoto hao wapo kwenye hatari ya kutofikia hatua timilifu ya ukuaji Kutokana na kuwa na viashiria mbalimbali ikiwamo vya udumavu na utapiamlo.

Programu ya MMMAM inatoa mchango katika kufanikisha Mpango wa Taifa wa Maendeleo ya Miaka mitano(2021/22-22025/26 ili kuleta jitihada za pamoja za wadau mbalimbali wakiwamo wa Afya, Elimu, Maendeleo ya Jamii, Lishe na asasi za kiraia kuangalia namba ya kuwasaidia Watoto hao Ili waweze kukua wakiwa na afya bora ambayo itawajenga katika mwili na akili.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...