Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa
mgeni Rasmi katika kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa Hayati baba wa
Taifa Mwalimu Julius Nyerere ambayo inatarajiwa kufanyika katika chuo
cha Uongozi cha mwalimu Nyerere kilichoko Kibaha mkoani Pwani.
Akizungumza
na waandishi wa habari mkoani Pwani ,Mkuu wa mkoa huo Abubakari Kunenge
amesema sambamba na kumbukizi hiyo ya baba wa Taifa Chama cha
Mapinduzi mkoa wa Pwani kimeandaa mdahalo .
Mdahalo huo una lengo la kutafakuri maisha ya mwalimu Nyerere ambao utafanyika April 9 mwaka huu katika chuo hicho.
Kunenge amebainisha,kila april 13 huwa kumbukizi ya kuzaliwa safari hii ,kumbukizi hii itatimiza miaka 100 ya mwl.Nyerere.
Hayati
Baba wa Taifa Mwalimu Julias Nyerere alizaliwa April 13 , mwaka 1922
kijijini Butiama mkoa wa Mara, na amefariki dunia mwezi October mwaka
1999.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...