Na WAF - Dodoma.
Imeelezwa kuwa tabia bwete (kutokushughulisha mwili kwa kufanya mazoezi) kuwa ni chanzo cha ongezeko kubwa la watu wenye magonjwa yasiyoambukiza nchini.
Dkt Ubuguyu amesema hayo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma alipokwenda kuzindua Mpango wa Kuzuia Madhara ya Kisukari kwenye Macho.
Amesema mabadiliko hasa kwenye maendeleo ya watu yanachagiza kukua kwa tabia bwete na kutoishughulisha miili kwa kufanya mazoezi, kutozingatia mlo kamili na kula kupita kiasi, matumizi ya vinywaji vyenye kilevi kupindukia pamoja na matumizi ya tumbaku.
Dkt. Ubuguyu amesema kuwa tafuti zinaonyesha kuwa asilimia 29 ya Watanzania ni wanene kupita kiasi kutokana na kula kupita kiasi hasa kwa watu wazima.
Tanzania inakadiriwa kuwa takriban asilimia 5.7 ya watu wenye umri wa miaka 20 hadi 79 wana ugonjwa wa kisukari. Tafiti zilizofanyika hapa nchini zimeonyesha kuwa asilimia 35 ya watu wenye kisukari wana madhara ya ugonjwa kwenye macho na asilimia 1 ya watu hao hupata ulemavu wa kutokuona au uoni hafifu.Daktari
bingwa mshauri wa macho kutoka Hospitali ya Raigmore Dkt. Rose Brennan
akionesha kamera ya kupima retina ya macho mbele ya Mkurugenzi wa huduma
za kinga Dkt. Omary Ubuguyu na Mkurugenzi mtendaji wa Hospitali ya
Benjamin Mkapa Dkt. Alphonce Chandika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...