Na WAF - Dodoma.
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba kutoka Wizara ya Afya Dkt. Omary Ubuguyu ameagiza kliniki za magonjwa yasiyoambukiza nchini kuwa na utaratibu wa kuwachunguza pazia la macho (Retina) wagonjwa wa Saratani.
Dkt Ubuguyu amesema hayo leo alipokuwa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa akizindua Mpango wa Kuzuia Madhara ya Kisukari kwenye Macho.
"Kila mgonjwa mpya wa Kisukari ni lazima apimwe macho kuona hali ya pazia la jicho (Retina) kwa wakati huo likoje na yule ambaye hana changamoto basi angalau na apimwe mara moja kila mwaka" amesema Dkt. Ubuguyu.
Dkt. Ubuguyu amesema kuwa Tanzania inakadiriwa kuwa takriban asilimia 5.7 ya watu wenye umri wa miaka 20 hadi 79 wana ugonjwa wa kisukari. Tafiti zilizofanyika hapa nchini zimeonyesha kuwa asilimia 35 ya watu wenye kisukari wana madhara ya ugonjwa kwenye macho na asilimia 1 ya watu hao hupata ulemavu wa kutokuona au uoni hafifu
Dkt. Ubuguyu amesema kuwa Wizara ipo kwenye mkakati wa utoaji mafunzo kwa watoa huduma ngazi ya huduma ya msingi ili waweze kutoa huduma stahiki kwa wateja wenye magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo uchunguzi wa madhara ya Kisukari kwenye Macho (Diebetic Retinopathy)
Aidha Dkt. Ubuguyu amemshukuru Dkt. Rosemary Brennan ambaye ni Daktati Bingwa kutoka Hospitali ya Raigmore kutoka Scotland pamoja na wadau wote nchini waliofanikisha kupatikana kwa kamera maalum kwa ajili uchunguzi wa madhara ya kisukari kwenye macho.

.jpeg)


.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...