Na.Khadija Seif, Michuzi TV
KAMPUNI ya Kuagiza Magari nchini (EZY Automotors) imeendelea kuwahakikisha wateja wake usalama na uwepesi katika Kuagiza gari nje ya nchi Huku wakitambulisha Huduma ya kukata bima ya Magari kama zawadi Kwa wateja wao.
Akizungumza na Michuzi Tv, Mkurugenzi mwenza wa Kampuni hiyo Mahsein Awadh maarufu kama dkt.Chen amesema Kampuni hiyo imejikita zaidi katika kuhakikisha Kila mtu ana miliki usafiri wake Ili kuendana na Kasi ya kukuwa Kwa miji na kurahisisha upatikanaji wa usafiri wa haraka zaidi.
Hata hivyo dkt.chen amesema Kwa wamama wenye vikundi vya kukopeshana Fedha na kuwekeza (vikoba) wafanye mchakato wa kumiliki gari Kwa ajili ya Biashara ili kuwahakikisha pesa waliyoiwekeza Inazaa matunda na kujenga uwaminifu kuepuka kutumia pesa hiyo kwenye anasa.
"Wamama Wenye vikundi wanaweza kuchagua kati ya kuwekeza Fedha na Kuagiza gari ya Biashara na Chombo hicho kikiwa Barabarani wanaweza kukusanya pesa hizo na kulipia kidogo kidogo mpaka kukamilika Kwa deni hilo Kwa muda wa miezi 6 au 12 wanaweza kuchagua masharti hayo.
Pia ameeleza kuwa kutokana na kupanda Kwa baadhi ya vitu hapa nchini Kuna baadhi ya Magari yataweza kupanda bei lakini mengine yatasalia Kwa bei Ile Ile kutokana na sehemu yanapoagizwa kutobadilika Kwa Mfumo wowote ule.
Mkurugenzi mwenza wa Kampuni ya EZY Automotors Mahsein Awadh maarufu kama dr.chen akizungumza na Waandishi Wahabari wakati wa kutembelea egesho la Magari mapya yaliyoingia nchini la Kampuni hiyo na kuwasihi wamama wavikoba kuhakikisha wanaagiza magari ya Biashara ili waweze kutumia Fedha walizowekeza katika vikundi vyao kuwekeza kwenye biashara yenye tija na uhakika Ili kuendelea kusukuma gurudumu la Maendeleo yao na Taifa Kwa ujumla
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...