Na Mwandishi Wetu, Michuzi Tv

Naibu Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalam,  Profesa Patrick Nsimama  leo amewaaga timu ya wanafunzi 21 na mwalimu mmoja ambao wanaelekea Meru nchini Kenya kwaajili ya mpango wa kubadilishana wanafunzi na walimu (exchange program).

DIT na Meru National Polytechnic wamesaini makubaliano ya kushirikiana katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na kubadilishana ujuzi na uzoefu ambapo wanafunzi na walimu kutoka Meru watakuja DIT na wa DIT kwenda Meru.

Makubaliano hayo yameingiwa na DIT kupitia Mradi wa EASTRIP unaofadhiliwa na Benki ya Dunia kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Mradi huo unaolenga kuboresha utoaji wa mafunzo ya elimu ya ufundi katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki zikiwemo Kenya,Tanzania na Ethiopia.

Wanafunzi wa DIT watakua katika chuo hicho kwa siku 14 ambapo watajifunza vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na utengenezaji 'Gypsam' pamoja na mapambo katika nyumba. Wanafunzi 25 kutoka Meru pia watakua DIT kwa siku hizo 14.

Akizungumza na time hiyo ya wanafunzi, Profesa Nsimama amewataka wanafunzi hao kwenda kuimarisha ushirikiano, kulinda heshima ya Taasisi na nchi kwa ujumla.

Aidha, amewataka pia kwenda kutekeleza kile kilichowapeleka wakitambua kuwa nafasi waliyoipata ni muhimu sana kwa manufaa yao na ya Taasisi. 




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...