Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Dkt Julius Kenneth Ningu amesema atafuatilia utendaji kazi kwa vijana walioteuliwa kufanya kazi ya usajiri wa anuani za makazi na postikodi
Dkt Ningu aliyasema hayo katika ukumbi wa shule ya sekondari Nasuli wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa vijana waliopata ajira ya muda katika zoezi la usajiri wa anuani za makazi na postikodi na uelezaji wa majukumu ya watendaji wa kata,vijiji, majukumu ya wenyeviti wa vijiji na wenyeviti wa vitongoji au mitaa katika zoezi hilo.
Aidha Dkt Ningu alidai uteuzi wa vijana hao umefanywa kwa umakini mkubwa hivyo ameahidi kuwafuatilia ili kuona weledi na uchapakazi walionao katika zoezi hilo ili kuona namna wanavoweza kutumia nafasi waliyopata kuitendea haki kikamilifu.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Chiriku Hamisi Chilumba amewaagiza watendaji wa kata,vijiji na vitongoji wa vijiji kuhakikisha wanawajibika katika nafasi zao ili kufanikisha zoezi la usajiri wa anuani za makazi na postikodi.
Chilumba pia aliwataka vijana walioteuliwa katika zoezi hilo kufanya kazi kwa bidii na kujituma ili kuwajengea viongozi wa wilaya imani ya kuendelea kuwaamini katika kazi zingine kama watafanya kazi hiyo kwa weledi na kwa kujituma .
Mratibu wa anuani za makazi na postikodi wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Saimon Sambalu alisema zoezi la usajiri wa anuani za makazi na postikodi litafanyika kwa weledi na umakini na kuhakikisha zoezi hilo litakwisha kabla ya wakati uliowekwa na serikali alisema Sambalu.
Maufunzo hayo katika wilaya ya Namtumbo yalifanyika katika kanda tatu ,kanda ya Mkongo.kanda ya Hanga na kanda ya Namtumbo kwa lengo la kupunguza msongamano wa kuwakusanya watu wengi katika eneo moja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...