Makambako
Jamii
nchini imeombwa kuwasaidia wanafunzi wa kike wanaoishi katika mazingira
magumu kwa kuwawezesha taulo za kike ili waepukane na adha ya kukosa
masomo pindi wanapokuwa katika siku zao (hedhi)
Wakizungumza
mara baada ya kupokea msaada huo, wanafunzi wa shule ya msingi
Kitandililo iliyopo halmashauri ya mji wa Makambako mkoani Njombe mara
baada ya kukabidhiwa taulo za kike na nguo za ndani na kikundi cha
chagua kurudisha tabasamu ambazo watatumia kwa kipindi cha miezi
sita,wamesema wengi wao wamekua wakishindwa kufika shule pindi
wanapokuwa hedhi kutokana na kukosa vifaa vya kujisitiri na kusababisha
kuchekwa na wezao.
Mwalimu
mkuu shule ya msingi Kitandililo Fatuma Kimbwanda amesema kutokana na
wanafunzi hao kukosa taulo imesababisha wengi wao kutumia vitambaa
ambavyo si salama kwa afya zao na kuwalazimu kutohudhuria masomo pindi
wanapokua hedhi.
Awali
wakikabidhi taulo hizo za kike na nguo za ndani kwa wanafunzi hao
wanaoishi katika mazingira magumu shule ya msingi Kitandililo wanachama
wa kikundi cha chagua kurudisha tabasamu akiwemo mwenyekiti wa kikundi
hicho Dafroza Kyando na Loyce Kaunda wamesema lengo lao ni kuhakikisha
watoto wa kike ambao wanaishi katika mazingira hatarishi wanasaidiwa ili
waweze kuhudhuria shule kama ilivyo kwa wanafunzi wengine.
Utafiti
ambao umefanyika mwaka 2015 na shirika la Netherlands development
pamoja na Tanzania water sanitation network katika halmashauri za
sengerema,Mufindi,chato na temeke ulionyesha asimilia 48 ya wanafunzi wa
kike hukosa masomo wanapokuwa hedhi.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...