Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akimkabidhi Nyaraka Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. George Simbachawene kama ishara ya kumkabidhi rasmi ofisi za Mji wa Serikali Mtumba Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. George Simbachawene alipowasili rasmi katika Ofisi yake kwa hafla ya makabidhiano ya ofisi Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga akizungumza wakati wa hafla hiyo.

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Mhe. George Simbachawene wakiweka saini nyaraka za makabidhiano ya ofisi ya Waziri Mkuu wakati wa hafla hiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. George Simbachawene alipowasili rasmi katika Ofisi yake kwa hafla ya makabidhiano ya ofisi Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Mhe. George Simbachawene (wa pili kushoto), Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (wa pili kutoka kulia), Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe.Ummy Nderiananga (wa kwanza kushoto) na Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Dkt. John Jingu (wa kwanza kulia) wakiwa katika picha ya Pamoja na watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu mara baada ya hafla ya makabidhiano iliyofanyika Jijini Dodoma.

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amekabidhi rasmi ofisi kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge Mhe. George Boniface Simbachawene ili kuendelea na majukumu katika ofisi hiyo.
Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya ofisi hiyo Aprili 02,2022 iliyofanyika katika Ofisi ya Waziri Mkuu zilizopo Mji wa Serikali Mtumba, Jijini Dodoma Mhe. Balozi Chana alimshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na kumhamishia katika Wizara ya Maliasili na Utalii huku akiwashukuru watendaji na watumishi wote wa Ofisi hiyo kwa ushirikiano waliompatia kwa kipindi chote alichohudumu katika Ofisi ya Waziri Mkuu.
Pia alitumia fursa hiyo kuendelea kuwakumbusha watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu kutekeleza majukumu yao kwa kwa weledi na ufanisi katika kuratibu shughuli za serikali na kumpatia ushirikiano Waziri mpya aliyepewa kuhudumu katika nafasi hiyo ili kuendelea kuiletea Nchi maendeleo.
“Niwashukuru sana kwa ushirikiano ambao mmenipa, na mapokezi tangu nimefika tumekuwa tukishirikiano katika mambo mengi sana mnanishauri, mnanielekeza, mnaniongoza na tuendelee na moyo wa kuchapa kazi chini ya Mheshimiwa wetu Waziri Mkuu,”Alishukuru Dkt. Pindi.
Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na kumteua kutumikia nafasi hiyo huku akiahidi kufanya kazi kwa bidii na wepesi wa hali ya juu ili kuhakikisha Ofisi hiyo inaendelea kuwa ya mfano kwa shughuli inazozitekeleza huku akiwaomba watendaji kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Sita inayohitaji matokeo.
“Serikali ni timu moja uwe unafanya kazi yoyote ndani ya serikali wewe ni timu ile ile kwa hiyo lazima twende kulingana na maono ya viongozi wetu wakuu ili yakitimia basi watanzania wote wananufaika na Wizara hii ndiyo inabeba maana ya serikali lakini ofisi hii ndiyo yenye matokeo lazima tufanye kazi kwa moyo na maono,”Alisema Mhe. Simbachawene.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...