Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Legal Services Facility (LSF), Lulu Ng’wanakilala akizungumza na wadau wa sekta ya msaada wa kisheria nchini (hawapo pichani) wakati wa kufunga Kongamano la Msaada wa Kisheria 2022 lililofanyika hivi karibuni Jijini Dodoma.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Legal Services Facility (LSF), Lulu Ng’wanakilala (kulia) akikabidhi mfuko wenye hotuba fupi kuhusu masuala mbalimbali yaliyojadiliwa na wadau wa sekta ya msaada wa kisheria nchini kwa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Geofrey Pinda wakati wa kufunga Kongamano la Msaada wa Kisheria 2022 lililofanyika hivi karibuni Jijini Dodoma.
Mratibu wa Mtandao wa Watoa huduma za Msaada wa Kisheria na Wasaidizi wa Kisheria nchini (Tanzania Paralegals Network - TAPANET), Tolbert Mmasy, akisoma hotuba fupi kuhusu masuala mbalimbali yaliyoazimiwa na wadau wa sekta ya msaada wa kisheria mbele ya Mgeni Rasmi, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria nchini, Geofrey Pinda, wakati wa kufunga Kongamano la Msaada wa Kisheria 2022 lililofanyika hivi karibuni Jijini Dodoma.
Msaidizi wa Kisheria kutoka Shirika la Msaada wa Kisheria Wilaya ya Kinondoni, Anthony Isakwi, akitoa mapendekezo yake namna ya kuboresha zaidi sekta ya msaada wa kisheria wakati wa kufunga Kongamano la Msaada wa Kisheria 2022 lililofanyika hivi karibuni Jijini Dodoma.
Katika picha ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria nchini Tanzania, Geofrey Pinda (katikati) na Katibu Mkuu Wizara hiyo, Mary G. Makondo. Wengine Msajili wa Huduma za Msaada wa Kisheria, Felistas Mushi (wa kwanza kushoto), Afisa Mtendaji wa Shirika la Legal Services Facility (LSF), Lulu Ng’wanakilala (wa pili kulia) na Mrajisi wa Mashirika Yasiyokuwa ya Kiserikali Zanzibar, Ahmed Khalid, wakati wa kufunga Kongamano la Msaada wa Kisheria 2022 hivi karibuni Jijini Dodoma.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Legal Services Facility (LSF), Lulu Ng’wanakilala (kushoto) akisalimiana na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria nchini, Geofrey Pinda, mara baada ya kuwasili kwenye Kongamano la Msaada wa Kisheria 2022 akiwa kama Mgeni Rasmi kwa ajili ya shughuli ya kufunga kongamano hilo lililofanyika hivi karibuni Jijini Dodoma.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...