Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambae ni mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara , NBC Premiere League jana iliipamba mechi ya watani wa jadi katika soka la Tanzania kati ya Yanga na Simba kwa kuandaa matukio kadhaa kwa ajili ya wapenzi wa mchezo huo pamoja na wateja wa benbki hiyo ikiwemo kukabidhi tuzo na zawadi kwa mchezaji bora na kocha bora wa mwezi Machi katika ligi hiyo.
Shughuli zote hizo ziliongozwa na maofisa waandamizi wa benki hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bw Theobald Sabi ambae alipata wasaa wa kukabidhi tuzo na zawadi ya fedha kiasi cha sh mil 1, kwa mchezaji wa klabu ya Simba Clatous Chama alietangazwa mchezi bora wa ligi hiyo kwa mwezi Machi sambamba na Kocha Mkuu wa Klabu hiyo Pablo Franco ambae pia alitangazwa kocha kwa mwezi huo na hivyo kuzawadiwa tuzo pamoja na fedha kiasi cha sh mil 1 kutoka kwa mdhamini huyo.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na maelfu ya mashabiki waliojitokeza kutazama mechi hiyo katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, lilitanguliwa na matukio mengine mengi ikiwemo mapokezi ya wateja wa benki hiyo kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini waliobahatika washindi katika Droo ya Jaza Kibubu Na NBC.
Washindi hao walipata fursa ya kushuhudia mechi hiyo wakiwa wamelipiwa gharama zote ikiwemo za usafiri, malazi sambamba na kupatikiwa tiketi za VIP kwa ajili ya kushuhudia mtanange huo uliomalizika kwa sare ya bila kufungana.
Pamoja na washindi hao benki hiyo pia iliandaa mwaliko rasmi kwa ajili ya wateja wake mashuhuri wakiwemo viongozi waandamizi kutoka mashirika na taasisi mbalimbali pamoja na wadau wengine wa benki hiyo waliopata wasaa kupata chakula cha mchana pamoja na viongozi wa benki ya NBC kisha kwa pamoja walielekea Uwanja wa Taifa kushudia mechi hiyo wakiwa katika msafara maalum.
Aidha, mashabiki waliojitokeza kutazama mechi hiyo walipata fursa ya kupata huduma mbalimbali za kifedha kutoka benki ya NBC kupitia maofisa wake mbalimbali waliokuwa wakitoa huduma hizo kwenye viunga vya vya uwanja huo, hatua iliyotoa fursa kwa mamia ya mashabiki hao kujiunga na huduma za benki hiyo ikiwemo kufungua akaunti mbalimbali pamoja na kufanya mihamala ya kifedha wakiwa maeneo hayo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambae ni mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara, NBC Premiere League Bw Theobald Sabi (Kushoto) akikabidhi hundi yenye thamani ya sh mil 1 kwa mchezaji wa klabu ya Simba Clatous Chama alietangazwa mchezi bora wa ligi hiyo kwa mwezi Machi wakati wa mechi kati ya Simba na Yanga iliyofanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam jana. Timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana. Anaeshuhudia ni Meneja Uhusiano wa benki hiyo, Godwin Semunyu (Kulia)
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambae ni mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara, NBC Premiere League Bw Theobald Sabi (Kushoto) akikabidhi tuzo kwa mchezaji wa klabu ya Simba Clatous Chama alietangazwa mchezi bora wa ligi hiyo kwa mwezi Machi wakati wa mechi kati ya Simba na Yanga iliyofanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam jana. Timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambae ni mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara, NBC Premiere League Bw Theobald Sabi (Kushoto) akikabidhi hundi yenye thamani ya sh mil 1 kwa kocha wa klabu ya Simba Pablo Franco alietangazwa kocha bora wa ligi hiyo kwa mwezi Machi wakati wa mechi kati ya Simba na Yanga iliyofanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam jana. Timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambae ni mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara, NBC Premiere League Bw Theobald Sabi (Kushoto) akikabidhi tuzo kwa kocha wa klabu ya Simba Pablo Franco alietangazwa kocha bora wa ligi hiyo kwa mwezi Machi wakati wa mechi kati ya Simba na Yanga iliyofanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam jana. Timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara kwa wateja wadogo na wa kati kutoka Benki ya NBC, Bw Elvis Ndunguru (kushoto) akiwaongoza wadau mbalimbali wa benki hiyo wakiwemo viongozi waandamizi kutoka mashirika na taasisi mbalimbali pamoja na wadau wengine wa benki hiyo kupata chakula cha mchana kabla ya kuelekea kutazama mechi kati ya Simba na Yanga.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambae ni mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara, NBC Premiere League Bw Theobald Sabi (Kushoto) akizungumza na mmoja wa wageni waalikwa wakati wa hafla ya chakula cha mchana kwa ajili ya wateja mashuhuri wakiwemo viongozi waandamizi kutoka mashirika na taasisi mbalimbali pamoja na wadau wengine wa benki hiyo kabla ya kuelekea Uwanja wa Taifa wa Benjamin Mkapa kushudia mechi hiyo wakiwa katika msafara maalum.
Msafara uliowabeba viongozi wa benki ya NBC pamoja na wadau mbalimbali wa benki hiyo ukifika Uwanja wa Taifa wa Benjamin Mkapa kushudia mechi hiyo.
Mashabiki waliojitokeza kutazama mechi hiyo walipata fursa ya kupata huduma mbalimbali za kifedha kutoka benki ya NBC kupitia maofisa wake mbalimbali waliokuwa wakitoa huduma hizo kwenye viunga vya vya uwanja huo, hatua iliyotoa fursa kwa mamia ya mashabiki hao kujiunga na huduma za benki hiyo ikiwemo kufungua akaunti mbalimbali pamoja na kufanya mihamala ya kifedha wakiwa maeneo hayo.
Zawadi mbalimbali kwa ajili ya mchezaji bora wa mwezi Machi pamoja na Kocha bora wa mwezi huo zikiingizwa uwanjani kwa ajili ya kukabidhiwa kwa wahusika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...