Serikali kupitia Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) imetoa kiasi cha shilingi bilioni nne nukta mbili (Bl 4.2)kujenga daraja jipya la Msadya lililopo kata ya Mwamapuli, Halmashauri ya Mpimbwe, Katavi.

Hayo yamebainishwa na Mtendaji Mkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seff katika ziara yake Mkoani Katavi ambapo leo Mei 20, 2020 ametembelea Halmashauri za Mpimbwe na Mlele.

”Ujenzi wa Daraja jipya la Msadya utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 4.2 na Mkandarasi Mshauri atakayesimamia atalipwa shilingi milioni 450. Kwa sasa mkandarasi analeta vifaa vyote hapa na tunategemea ataanza kazi baada ya wiki moja, “ alisema Mhandisi Seff.

Pia alieleza kuwa kazi ya ujenzi wa daraja hilo inategemewa kumalizika katika kipindi cha miezi 18.

Naye diwani wa kata ya Mwamapuli Mhe. Edward Nyorobi alisema kuwa daraja hilo linalounganisha kata za Mwamapuli na Chamalendi ni muhimu sana kwa wananchi kwa ajili ya kusafirisha mazao yao na kukuza shughuli za kibiashara na uchumi.

“Kata hizi zinategemewa sana kwa kuzalisha chakula na kukuza mapato ya hapa na Halmashauri nzima. Kuna hekta zaidi ya 13000 za uzalishaji wa mazao. Tunamshukuru sana Rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea pesa za daraja hili ambalo litakuwa mhimili na ukombozi kwetu, “ alisema Mhe. Edward.

Kwa upande wake ndugu Hansi Mwinga mkazi wa Mwamapoli alisema kuwa anaishukuru Serikali kwa kuwajengea daraja wanalotumia kwa sasa baada ya daraja la awali kuvunjika na kueleza kuwa daraja jipya litakalojengwa litakuwa ni suluhisho la kero zao za muda mrefu.

“ Tunachoiomba Serikali ni Kutujengea Daraja la viwango litakaloweza kubeba kuanzia tani 30 ili liwe na faida kubwa kwetu katika kusafirisha mazao,” alisema Hansi.

Alieleza kuwa daraja la awali lilikuwa na uwezo mdogo magari yakapita yenye tani nyingi jambo lililopelekea kuvujika kwa daraja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...