Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo ametoa agizo kwa viongozi wa chama ngazi zote nchi nzima, kuanzia Tawi, Kata, Wilaya, Mkoa na Taifa kushiriki vikao vya mashina ili kuendelea kuimarisha zaidi CCM, ambacho msingi wa uimara wake unaanzia hapo.

Aidha, Ndugu Chongolo kasema kuwa, baada ya Uchaguzi Mkuu wa CCM unaoendelea nchi nzima, chama kitandaa mafunzo maalum kwa ajili ya viongozi wa chama ngazi zote nchi nzima kuanzia mabalozi mikoa hadi taifa ili wote wajue wajibu, ukubwa wa nafasi waliopewa, dhamana walizonazo, maadili na mambo ya msingi ya nafasi walizonazo.

“Nitumie nafasi hii kuhamasisha na kutoa agizo muhimu kwa ngazi zote za uongozi kuanzia tawi, kata, wilaya, mkoa mpaka taifa tushuke chini kwenda kuwatembelea na kushiriki vikao vya mashina vya mabalozi, tukishuka huku chini tukashiriki vikao vyao tutajua changamoto, na tukijua tutashiriki utatuzi wake.”

Katibu Mkuu ameyasema hayo leo tarehe 30 Mei, 2022 katika Mkutano wa Shina Namba 6, Tawi la Negezi, Kishapu mkoani Shinyanga katika ziara yake inayoendelea ikiwa na lengo la kukagua na kuhamasisha uhai wa chama pamoja na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Aidha, kutokana na changamoto za baadhi ya miradi kuchelewa kukamilika kwa sababu ya uhaba wa fedha, Katibu Mkuu amezielekeza halmashauri kuacha kugawanya fedha katika miradi mingi na hivyo kushindwa kuikamilisha, badala yake, amezitaka zielekeze fedha katika miradi michache ya kipaumbele itakayotekelezwa kwa ukamilifu na kuleta matokeo yanayooneka na yenye tija kwa haraka

Katibu Mkuu ametoa maelekezo hayo wakati akikagua mradi wa daraja la Ipeja-Itilima wilayani Kishapu ambao umekamilika kwa gharama ya milioni 486.

“Sio mnapewa bilioni moja mnapeleka kwenye miradi 40, ambayo haikamiliki, hizo zama zimepita tunataka fedha zielekezwe kwenye mradi unaokwenda kukamilika kwa asilimia 100.

“Na sio fedha zitolewe kidogo kidogo zikafanye kazi kidogokidogo tija yake haionekani…hayo siyo mambo tunayotaka,” Katibu Mkuu Ndg. Chongolo amesisitiza

Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu baada ya kupokea changamoto ya barabara ya Kolandoto – Meatu, ameahidi kusukuma upatikanaji wa fedha kutoka mfuko wa dharura kugharamia ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 53.



Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akisalimiana na Elias Bush mwanachama aliyejiunga na Chama Cha Mapinduzi akitokea CHADEMA nje ya ofisi za CCM Kishapu.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akiangalia maendeleo ya ujenzi wa Wodi ya Mama na Mtoto katika Hospitali ya Wilaya ya Kishapu.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akiangalia maendeleo ya ujenzi wa Wodi ya Mama na Mtoto katika Hospitali ya Wilaya ya Kishapu, kushoto ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya Dkt. Mohamed Mkumbwa.



Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akiangalia maendeleo ya ujenzi majengo mbalimbali katika Hospitali ya Wilaya ya Kishapu, kushoto ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya Dkt. Mohamed Mkumbwa.


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akisikiliza kwa makini taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa Wodi ya Mama na Mtoto katika Hospitali ya Wilaya ya Kishapu,kutoka kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya Dkt. Mohamed Mkumbwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...