KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo ametoa muda wa mwezi mmoja kwa Bohari ya Dawa (MSD) kufanikisha upelekaji wa vifaatiba katika Hospitali ya Wilaya ya Ushetu Mkoani Shinyanga ili ianze kutoa huduma kwa wananchi.
Chongolo ametoa agizo hilo leo Mei 28,2022 wakati wa ziara yake ya kukagua jengo la Hospitali hiyo ya Wilaya ya Ushetu ikiwe ni muendelezo wa ziara zake katika Mikoa ya Shinyanga na Simiyu.
Amesema atazungumza na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kuhusu MSD kuchelewesha uletaji wa vifaatiba hivyo lakini pia amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Sophia Mjema kumtafuta mhusika wa Bohari ili aweze kukutana nae.
" Niagize ndani ya mwezi huu au mwezi ujayo hivyo vifaa viwe vimefika hapa ili vianze kutoa tiba na huduma kwa wananchi wetu, haiwezekani Rais wetu mpendwa Samia Suluhu Hassan anashusha fedha nyingi huku kuja kutengeneza miundombinu ya Kisasa halafu vifaatiba inakua ni hadhithi, hili halivumiliki.
Hatupo tayari kuona watu wachache wanakwamisha juhudi zinazofanywa za kuwahudumia wananchi wetu, CCM tuliahidi kupitia ilani yetu mwaka 2020 na tunatekeleza," Amesema Chongolo.
Awali Mbunge wa Ushetu, Emmanuel Cherehani alimueleza Katibu Mkuu Chongolo kwamba walipokea sh Bilioni 3.2 kwa ajili ya Hospitali hiyo lakini licha ya majengo baadhi kukamilika bado hawajaletewa vifaatiba na wahudumu kwa ajili ya kuhudumia wananchi wa Wilaya hiyo.
"Tunaomba Katibu Mkuu utusaidie kutusemea Hospitali imeshakamilika ila vifaatiba na wahudumu ndo changamoto, inatulazimu kuwapeleka wagonjwa zaidi ya km 40 hadi Kahama.
Majengo tayari tunachoomba utusaidie vifaatiba vifike pamoja na wahudumu wa Afya ili wananchi hawa wa Ushetu wasiwe wanatembea umbali mrefu kufuata matibabu," Amesema Cherehani.
Ujenzi wa Hospitali hiyo umetekelezwa kwa awamu tatu na ulianza January 2019 ambapo Serikali imepeleka fedha jumla ya Sh Bilioni 3.2 kwa ajili ya kukamilisha.
Picha mbalimbali zikionesha Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akikagua ujenzi wa jengo la utawala katika hospitali hiyo.PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-MMG
Muonekano wa jengo la Utawala wa hospitali hiyo ya Wilaya ya Ushetu mkoani Shinyanga.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akipata maelekezo kutoka kwa Mganga Mkuu wa Halmashauri ya. Wilaya ya Ushetu mkoani Shinyanga,Dk. Nicodemus Senguo wakati alipokagua akikagua ujenzi wa majengo mapya ya hospitali ya wilaya hiyo leo Mei 28,2022.
Moja ya jengo la hospitali hiyo likiendelea kujengwa
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo kimsikiliza Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM,Kanali Mstaafu Lubinga Ngemela wakati akitoa maoni yake katika ukaguzi wa ujenzi wa hospitali hiyo.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akzungumza jambo na msaidizi wake Bw. Saleh Mhando mara baada ya kufanya ukaguzi wa ujenzi wa jengo la utawala katika hospitali hiyo.
Wannachi wa kijiji cha Mtonga kata ya Nyamlingano wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo wakaati akizungumza nao mara baada ya kukagua ujenzi huo wa Hospitali ya Wilaya ya Ushetu mkoano Shinyanga.
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM, Kanali mstaafu Ngemela Lubinga akifafanua baadhi ya mambo katika kikao hicho.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akizungumza na wananchi wa Kijiji Cha Mitonga baada ya kukagua ujenzi wa jengo la utawala katika hospitali hiyo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...