Na Dotto Mwaibale, Dar es Salaam

MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), CPA Charles Kichere ameviomba vyombo vya habari kuandika habari za uchunguzi ili kusaidia Serikali kubaini mianya ya matumizi mabaya ya fedha za umma.

CPA Kachere ameyasema hayo wakati akitoa taarifa kwa wahariri wa vyombo vya habari wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kwaida wa kuwajengea uwezo ili waweze kujua shughuli mbalimbali zinazofanywa na ofisi ya CAG.

"Waandishi wa habari ni wadau wakubwa sana katika kuhabarisha jamii kuhusu shughuli mbalimbali tunazozifanya hasa katika eneo la utawala bora hivyo tunahitaji ushirikiano wenu" alisema Kachere.

Alisema waandishi wa habari wanakazi kubwa ya kimkakati wanayo ifanya katika jamii kama ilivyo mihimili mingine katika kuhabarisha umma habari mbalimbali kwa kuzingatia maadili ya kazi zao.

Akijibu maswali kuhusu  sheria ya manununuzi alisema imekuwa na changamoto kubwa na mapungufu kadhaa ambayo yanafanyiwa kazi na Serikali.

Alisema sheria hiyo inatakwa kufanyiwa mabadiliko ili kuisaidia Serikali na akasema wsimamizi wa sheria hizo wanatakiwa kuwa waadilifu ili kazi isonge mbele.

Akielezea kuhusu suala la mazingira alisema kuna kila sababu ya kuongeza nguvu katika eneo hilo na akakiomba chama cha waandishi wa habari za mazingira (JET) kuhamasisha jamii kuhusu uhifadhi wa mazingira na kuwa ofisi ya CAG itaongeza kasi ya ukaguzi vinginevyo nchi itageuka kuwa jangwa.

Alijibu suala la vitisho alisema ofisi yake haiogopi vitisho vya mtu yeyote kwani wanafanya kazi kwa uhuru na kwa mujibu wa sheria na wapo kwa jili ya kufanya kazi za Serikali na kuangalia maslahi ya Taifa na wananchi na kuwa wamekuwa na ushirikiano mzuri dhidi yao na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) hasa katika eneo la manunuzi.

Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), CPA Charles Kichere akizungumza  na Wahariri wa vyombo vya habari wakati akitoa taarifa ya ufunguzi wa mkutano wa kwaida wa kuwajengea uwezo ili waweze kujua shughuli mbalimbali zinazofanywa na ofisi ya CAG mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam leo..
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF)  Deodatus Balile akizungumza kwenye mkutano huo.
Mhariri Jackton Manyerere akizungumza kwenye mkutano huo.
'
Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Majira Emmanuel Mbuguni akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea
Wahariri wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...