Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
MKUU
wa Wilaya ya Kibaha, Sara Msafiri, ameamuru Mtendaji wa Kijiji Cha Ruvu
Stesheni Neema Shang'a ambae kwa Sasa kaamishwa kituo Cha kazi kufuatia
tuhuma zinazodaiwa kujichotea fedha za Kijiji kinyume na taratibu kiasi
cha sh.650,000 azirejeshe Mara moja .
Ameeleza
timu ya wakaguzi wa ndani ilifika katika Kijiji hicho miaka miwili
kuona matumizi na makusanyo Kama kinafuata taratibu za fedha ambapo
ilibaini kutolewa kwa fedha hizo .
Akizungumza
na wananchi wa Kijiji Cha Ruvu Stesheni, ambao walifikisha malalamiko
kutokuwa na mikutano ya vijiji na mapato na matumizi, Msafiri alieleza
wakati jarada linaendelea na uchunguzi na TAKUKURU kwanza mtendaji huyo
anapaswa kurudisha fedha za umma.
Aliwaasa watendaji wengine kuacha kufanya udokozi wa fedha za Kijiji kabla ya vikao vya kupitisha ili fedha itoke kihalali
Mkuu huyo wa wilaya alisema ,hatua hii iwe fundisho kwa wengine ,hata Kama kaamishwa kituo Lakini atume pesa za Kijiji .
"Sheria
za fedha zinaelekeza kwamba fedha yoyote ya umma unapoikusanya
usiitumie Mpaka upeleke kwenye akaunti ya Kijiji halafu matumizi yake
unaandikia hoja unapeleka katika vikao ambavyo vikipitisha ndio ifanyiwe
matumizi"
"Kuna fedha
zinatolewa zimetumika kinyume na Utaratibu, Sasa ripoti zimekamilika na
nimewaagiza wakaguzi wa ndani waje wasome ripoti hiyo ili penye
mapungufu na fedha zilizotumika wapewe elimu kamati ya fedha na mipango
ili mambo yasijirudie .
Alibainisha ,Kuna watendaji wanaamishwa ambao ripoti ya ukaguzi inaonyesha walifanya matumizi ya fedha kinyume na Utaratibu.
Msafiri
aliwaambia mkurugenzi,mwanasheria ,wakuu wa idara ,maofisa utumishi na
maofisa ununuzi popote kamati za Serikali za Vijiji zinapotoa hoja ya
matumizi ya fedha waende kusaidia Vijijini maana changamoto za miradi ya
Ruvu Stesheni zinatokana na mlundikano wa matatizo ambayo Serikali ya
Kijiji imefikisha ngazi ya halmashauri Lakini zinacheleweshwa kupatiwa
ufumbuzi.
"Na hii
inasababisha Mwenyekiti wa Kijiji anaogopa kuitisha mikutano ya wananchi
maana anakuwa Hana majibu ya kutoa kwa wananchi."
Awali baadhi ya wanakijiji walitoa kilio chao juu ya miradi ya maendeleo kukwama ikiwemo Zahanati ya Kijiji kutoanza kazi .
Kutokana
na changamoto hiyo Msafiri ,aliitaka Halmashauri ya wilaya ya Kibaha
,kwa Hali ya jengo ilipofikia kuhakikisha inafanya umaliziaji na kuanza
kutoa huduma Juni 25 mwaka huu.
Alitaka
,jengo lianze kutoa huduma za awali za mama mjamzito na watoto wakati
wakisubiri vifaa tiba na vyombo vya dola kuendelea na baadhi ya
uchunguzi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...