Diwani wa kata ya Kibedya Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro Butindi Masatu amekabidhi printa katika shule ya sekondari Kibedya ikiwa ni sehemu ya kutimiza ahadi yake aliyowahi kuitoa katika shule hiyo.

Akizungumza na Michuzi Blog Diwani huyo alisema printa hiyo itasaidia katika kuchapisha mitahani ya majaribio kwa wananfunzi ya mara kwa mara ili kuongeza kiwango cha ufauru kwa wanafunzi hao

Aidha aliwaomba walimu kutekeleza majukumu yao ili kumuunga mkono Mhe Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kwa kutatua na kushughulikia kero za watumishi ikiwa ni pamoja na kuongeza mishahara.

Masatu alisema printa hiyo imeghalimu shilingi milioni moja(1,000,000) ambapo amefanya hivyo ili kuongeza motisha kwa walimu waweze kufanya kazi kwa bidiii na kuongeza ufaulu kwa katika shule hiyo.

Kwa upande wake kaimu Mkuu wa shule ya Sekondari Kibedya Mwalimu Edsoni Mfaume alimshukuru Diwani kwa kuwapelekea Printer hiyo ambapo alisema itawasaidia katika kuongeza ufauru kwani wanafunzi watakuwa na mitihani ya majaribio ya mara kwa mara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...