Na Mwandishi wetu, Simanjiro
SHIRIKA
lisilo la kiserikali la ECLAT Foundation limekabidhi madarasa saba
yakiwemo matatu mapya na manne yaliyokarabatiwa ya shule ya msingi
Nakweni ya Kata ya Shambarai Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.
Pia,
ECLAT Foundation, imekabidhi madawati 69, ofisi mbili za walimu, viti
12 na meza 12 ambapo thamani ya miradi hiyo ni shilingi milioni 162.
Mwenyekiti
wa ECLAT Foundation, Peter Toima akizungumza baada ya kukabidhi mradi
huo amesema baada ya kuelezwa changamoto ya upungufu wa madarasa
waliamua kuyafanyia kazi.
Amesema
shirika la ECLAT Foundation limefanya mambo mengi kwa ajili ya manufaa
ya jamii japokuwa hawajigambi wala kutamba kwani wanasaidia wananachi.
"Sisi
na shirika la Ujerumani la Upendo tulipopata taarifa ya mapungufu ya
shule hii tuliweka mikakati na kufanikisha ujenzi wa miundombinu hii,"
amesema Toima.
Mkuu wa
wilaya ya Simanjiro Dk Suleiman Serera amewapongeza wana Kijiji wa
Nakweni kwa kuanzisha mradi huo kwani endapo wasingeanzisha ECLAT
wasingeumaliza na kujenga mingine.
Hata hivyo amewataka wanafunzi, walimu, wazazi na walezi wa shule hiyo kutunza miundombinu hiyo kwa ajili ya manufaa yao.
"Baada
ya mradi huu kukabidhiwa kwenu mnapaswa kuitunza kwani wakati wa
ukaguzi nimeona darasa moja limechorwa na wanafunzi," amesema Dk Serera.
Mwalimu
mkuu wa shule hiyo Namweli Chao amesema shule hiyo ilianzishwa baada ya
wanafunzi wa kijiji hicho kutembea umbali mrefu kufuata elimu maeneo
mengine.
"Wanafunzi
walikuwa wanatembea kilomita 22 hadi kijiji cha Kilombero au kilomita 18
kwenye kijiji cha Olbili kwenda kusoma kwenye shule za msingi na kurudi
kwa kilomita hizo," amesema Chao.
Mwanafunzi
wa darasa la sita wa shule ya msingi Nakweni, Esupati Ngidutu amesema
awali wanafunzi wa madarasa mawili walikuwa wanatumia chumba kimoja
kusoma.
Mwanafunzi wa
darasa la tano wa shule hiyo Saruni Ikoyo amemshukuru Toima Mwenyekiti
wa ECLAT Foundation kwa kufanikisha ujenzi wa madarasa hayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...