NA YEREMIAS NGERANGERA..NAMTUMBO
Viongozi wa Jumuiya za watumiaji maji katika wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma zimepata mafunzo ya siku moja kuwawezesha kufanya kazi zao kwa kuzingatia sheria ,kanuni , taratibu na miongozo iliyowekwa na serikali .
Akifungua mafunzo hayo mkuu wa wilaya ya Namtumbo Dkt Julius Kenneth Ningu aliwataka washiriki wa mafunzo kuzingatia mafunzo hayo na kisha kwenda kutumia maarifa watakayoyapata katika kazi zao za kila siku .
Awali mratibu wa mafunzo kwa jumuiya za watumiaji maji RUWASA wilayani Namtumbo George Mswaya alisema washiriki wa mafunzo hayo ni viongozi wa jumuiya za watumiaji maji kutoka katika vijiji ,kata vya wilaya ya Namtumbo.
Mswaya aliwataja watendaji wa kata ,makatibu ,wahasibu na mafundi wa jumuiya za watumiaji maji katika wilaya hiyo kuwa ni washiriki wa mafunzo hayo ili kuwajengea uwezo wa kiutawala katika kuimarisha jumuiya zao .
Viongozi wa jumuiya za watumiaji maji walifundishwa mada tano(5) ikiwemo ya utunzaji sahihi wa fedha iliyofundishwa na mhasibu wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Obed Mwasomola ,mada ya mazingira iliyofundishwa na afisa mazingira wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Kelvin Mnali ,mada ya sheria ya huduma ya maji na usafi wa mazingira iliyofundishwa na mwanasheria wa Halmashauri hiyo Fabian Samweli na mada ya umuhimu wa kuchangia ankra za maji ikifundishwa na afisa maendeleo ya jamii wa Halmashauri hiyo Jesca Mwitinda.
Aidha mhandisi wa RUWASA wilaya ya Namtumbo David Mkondya aliwasisitizia washiriki wa mafunzo kwenda kuongeza watumiaji maji katika jumuiya zao, kwenda kuhakikisha jumuiya zao zinasajiriwa kisheria,kwenda kuhakikisha jumuiya zao zinakuwa na viongozi wanawake na kuhakikisha katika huduma za maji kunakuwa na mfumo wa kutibu maji kwa lengo la kutimiza vigezo vilivyowekwa na wafadhili wanaoshindanisha watumiaji maji, na jumuiya ya watumiaji maji inayokidhi vigezo hulipwa 56,250kwa kila mtumiaji maji katika jumuiya iliyokidhi vigezo hivyo.
Yasini Salumu Kayonga fundi na katibu wa bodi ya maji katika jumuiya ya kijiji cha matepwende Pamoja na kuipongeza RUWASA kwa kuwapa mafunzo hayo alidai mafunzo hayo yameongeza ari ya kufanya kazi kwa kuzingatia sheria,kanuni ,taratibu na miongozo iliyowekwa na kuwafanya washiriki kwenda kufanya kazi zao kwa kujiamini alisema Kayonga.
Mafunzo kwa viongozi wa jumuiya za watumia maji wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma yalifunguliwa na mkuu wa wilaya ya Namtumbo Dkt Julius Kenneth Ningu katika ukumbi wa UNICEF uliopo katika kijiji cha Mkongo gulioni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...