Na Mashaka Mhando,Muheza
HEKTA 8,000 za mazao mbalimbali wilayani Muheza, zimeshambuliwa na wadudu waharibifu wajulikanao kwa jina la Viwavijeshi.
Kufuatia
hali hiyo, Mbunge wa Muheza Hamis Mwinjuma maarufu MwanaFA, ameishukuru
serikali baada ya kumpa lita 86,000 za sumu aina ya Power-Cron
itakayokabiliana na uharibifu huo.
Akizungumza
wakati akizindua zoezi la usambazaji wa dawa hizo, alisema mara baada
ya kutokea wadudu hao na wakulima kulalamika, alifikisha kilio chao kwa
kuomba dawa yenye viuwatilifu vya kukabiliana na wadudu hao kwa Waziri
wa Kilimo Hussein Bashe.
"Namshukuru
Waziri Rais wetu Samia Suluhu Hassan, kiukweli dawa hii itatusaidia
kupambana na wadudu hawa mashambani," alisema mbunge.
Hata
hivyo, mbunge alisema anapanga kukutana na makundi ya wakulima ili
aweze kuzungumza nao kutazama namna ya kutatua changamoto zao.
"Nataka
kukutana na wakulima lengo ni kuwabadilishia maisha yawe bora zaidi
kuliko jana na leo, kwa kuzalisha mazao bora na masoko ya uhakika,"
alisema MwanaFA.
Mwenyekiti
wa halmashauri ya wilaya ya Muheza, Erasto Mhina amemshukuru mbunge kwa
jitihada za kupata dawa hiyo ambayo itaokoa mazao yalikuwa
yameshambuliwa na wadudu hao.
Ofisa
Kilimo wilayani Muheza, Hoyange Mbwambo, alisema kuwa sumu hiyo aina ya
Power-Cron imeanza kusambazwa kwa wakulima ili kukabiliana na wadudu
hao waharibifu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...