*Wajumbe wa Kamati wapongeza DART kwa ufanisi wa kazi, DART na UDART watakiwa kukutana na kamati hiyo kunoana
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
WAKALA wa Usafiri wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) umesema kuwa usafiri wa
mabasi yaendayo haraka kwa Barabara kuanzia Mbagala kuelekea Gerezani
kuanza Machi 23.
Hayo
ameyasema Mtendaji Mkuu wa DART Dk.Edwin Mhede wakati Kamati ya
Bunge ya Utawala wa Serikali za Mitaa na Kamati ya Bunge ya Utawala wa Serikali za Mitaa (USEMI) ilipotembelea
mradi huo jijini Dar es Salaam kwa kuangalia mifumo mbalimbali ya
Wakala huo.
Dk.Mhede
amesema wakala huo unajivunia mifumo ya ukusanyaji mapato ambapo
imeongezeka kutoka sh.bilioni 1.8 hadi kufikia sh.bilioni Tatu kwa
Mwezi.
Amesema mifumo hiyo imetengenezwa na wataalam ambao ni watanzania ambapo umesaidia kuokoa fedha ya serikali.
Aidha
Dkt.Mhede amesema kuwa malengo ambayo wamejiwekea ni kuhakikisha
wanakwenda kutoa huduma bora ya usafiri katika jiji la Dar es Salaam
ambayo itachochea na uchumi kukua.
Kamati
hiyo baada ya kupata taarifa za DART imeiagiza DAR na UDART kukutana
na kamati hiyo na kuwapa maelezo ya kina pamoja na sheria ilioanzisha
mradi huo ambapo ndipo wanaweza kushauri serikali kama kuna jambo la
kufanya.
Mwenyekiti
wa Kamati hiyo Abdallah Chaurembo ambaye ni Mbunge wa Mbagara amesema
kuwa mradi huo uko vizuri na kushauri waendelee kuboresha baadhi ya
kasoro.
Mjumbe
wa Mjumbe wa Kamati na Mbunge wa Urambo Magreth Sitta ameiopongeza DART
kwa kazi nzuri wanayoifanya katika utoaji wa huduma ya usafiri katika
jiji Dar es Salaam.
Nae
Mjumbe wa Kamati hiyo Mwantum Haji amesema kuwa DART wanafanya kazi
nzuri ambayo matokeo yake yanaonekana katika usimamizi wa maradi huo na
kuongeza kuwa wanaupiga Mwingi.
Mtendaji Mkuu wa DART Dk.Edwin Mhede akizungumza wakati Kamati ya Bunge ya
Utawala wa Serikali za Mitaa na Serikali za Mikoa (USEMI) ilipotembelea
Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Bunge ya Utawala wa Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa
Abdallah Chaurembo wakifurahi jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa DART
Dk.Edwin Mhede mara baada Dk.Mhede kumkabidhi zawadi ya kikombe kwa
niaba ya Kamati nzima
Kamati
ya Bunge ya Utawala wa Serikali za Mitaa na Serikali za Mikoa
(USEMI)wakipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa DART Dk.Edwin
Mhede wakati wa ziara ya kamati katika Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka
jijini Dar es Salaam.
Kamati ya Bunge ya USEMI ikiwa katika ziara ya miundombinu mbalimbali ya DART.
Kamati
ya Bunge ya Utawaka Serikali za Mitaa na Tawala Mikoa (USEMI) wakipata
maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Usafirishaji wa DART
Mhandisi Fanuel Kalugendo akitoa maelezo huhusiana na miundombinu ya
huduma za usafirishaji wa abiria katika jiji la Dar es Salaam.
Kamati
ya Bunge ya Utawala wa Serikali za Mitaa na Serikali za Mikoa (USEMI)
wakiwa katika usafiri wa mabasi yaendayo haraka wakati kamati hiyo
ilipotembelea Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...