Chura huyu anaitwa Chura wa Kihansi kwa lugha ya kiingereza anaitwa “Kihansi Spray Toad” na kwa kitaalamu anaitwa “Nectophrynoides asperhinis” ni moja ya bionuai muhimu za kuhifadhi na hapatikani sehemu nyingine yeyote duniani isipokuwa katika bonde la Kihansi nchini Tanzania.
Chura wa Kihansi ni chura pekee katika jamii ya vyura waliopo duniani kwani hawa vyura hutaga mayai na kukaa nayo kwenye kifuko kilichopo kwa chura huyo hadi yanapoanguliwa na kutoa vitoto hai.
Swala la kuangua vyura hai wakati jamii nyingine za vyura hutaga mayai na kuyaacha majini ambako huanguliwa wakati mama yao hayupo inamfanya chura huyu kuwa wa kipekee duniani.
Makazi na maisha ya chura huyu pamoja na viumbe wengine ni kiashiria cha mazingira bora,hivyo kupotea kwa chura pamoja na viumbe wengine kama kahawa pori na kipepeo waliopo katika bonde hili ni ishara ya uharibifu wa mazingira na Bionuai.
Vyura hawa wa Kihansi wako chini ya Usimamizi na uhifadhi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania(TAWA) wakishirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania(TAWIRI) kwenye utafiti wa hao vyura.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...