Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Nahodha wa Young Africans SC, Bakari Nondo Mwamnyeto rasmi ameongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuitumikia Klabu ya Soka ya Yanga baada ya mkataba wake wa awali kuisha katika Klabu hiyo.

Mwamnyeto ameongeza miaka miwili kuwatumikia Wananchi baada ya kuonyesha kiwango bora katika Kikosi hicho licha kuwepo kwa tetesi kuwa Beki huyo anawaniwa na Watani wa Jadi, Simba SC katika msimu ujao wa mashindano.

Yanga SC wamethibitisha hilo kumuongeza mkataba Mwamnyeto baada ya kuchapisha picha zikionyesha Nahodha huyo akisaini na kuthibitisha kubaki klabuni hapo kwa misimu mingine miwili ya mashindano.


“Wananchi wenyewe wameshasema, mimi nani nikatae? bado nipo hapa kuongoza Jahazi la Wananchi, naitwa Bakari Mwamnyeto Nondo, bado nipo Yanga SC miaka mingine miwili”, amesikika Mwamnyeto.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...