Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV


WAZIRI wa Habari,Mawasiliano na  Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amefika Temeke kukagua maendeleo ya zoezi la anwani za makazi lililoendeshwa Tanzania nzima.

Nape amefika wilayani Temeke akiwa  ameambatana na wenyeji wake ambao ni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam mheshimiwa Amos Gabriel Makalla,naibu waziri wa TAMISEMI David Silinde,mkuu wilaya  Jokate Mwegelo,Meya Abdallah Mtinika,Mkurugenzi wa manispaa Elihuruma Mabelya pamoja na wakuu wa idara na taasisi mbalimbali.

Katika kikao hicho waziri Nape aliwapongeza viongozi wa Wilaya na Manispaa kwa kusimamia vema utekelezaji wa "Oparesheni hiyo". waziri Nape aliendelea kusisitiza kuwa licha ya kufanya vizuri viongozi na watendaji waendelee kushirikiana kumalizia kazi iliyosalia ya uwekaji vibao na nguzo.

"Nashukuru na kukupongeza Mkuu wa mkoa na Viongozi wengine, haikua kazi rahisi lakini mpaka sasa Nchi nzima tumefikia asilimia 94%,Dar es Salaam mmenipa amani zoezi mmeliendesha vizuri sana kwa sehemu ya kwanza,ukiona Temeke imefanikiwa ujue Dar es Salaam imefanikiwa,mna kiongozi imara, Mhe. DC Jokate anafanya kazi"

Aidha Waziri  Nape amewataka viongozi kuhakikisha wanamalizia sehemu iliyobaki ya kuweka vibao ndani ya mwezi huu (Mei) zoezi ambalo limeshaanza katika baadhi ya maeneo na kuhakikisha miundombinu inalindwa.

"Zoezi litakapokamilika tuhakikishe miundombinu inalindwa dhidi ya waharibifu,ikumbukwe kwamba anwani za makazi zinakwenda kuiweka Tanzania kidijitali,zitatusaidia wenyewe hata kwenye kuelekezana kawaida,kwenye masuala ya ulinzi na usalama,masuala ya kibenki na mengineyo,tukaitunze miundombinu hiyo,”alisema Waziri Nape.

Kwa upande wake Naibu waziri wa TAMISEMI David Silinde alisema Wananchi waendelee kushirikishwa katika kila hatua ya kufanikisha zoezi la anwani za makazi.

"Anwani za makazi ni jambo linalowahusu Wananchi na TAMISEMI ipo,mmefanikiwa kwenye ukusanyaji mkafanikiwe na kwenye kukamilisha kwa wakati uwekaji wa vibao haya ni maagizo ya waziri wa TAMISEMI,hii inawahusu TARURA pia, kwa kushirikiana na Halmashauri tumieni hata mapato yenu ya ndani kukamilisha zoezi hili"

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam  Amos Makalla alitoa pongezi kwa waziri Nape, viongozi na watendaji kwa kufanikisha zoezi kwa ushirikiano mkubwa.
"Anwani za makazi tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa huu ulikua mzigo mkubwa kwako Mheshimiwa Waziri lakini umeweza kuubeba,hatukua na uelewa wa " postcode" ukiambiwa jaza postcode huelewi uweke namba ya simu au anwani ya posta lakini sasa tumefanikiwa kwenye hilo" alisema Makalla

Baada ya kukagua zoezi katika mtaa wa Wailes waziri Nape aliwakumbusha Wanatemeke kutunza miundombonu na kuwa tayari kwa zoezi la sensa ya watu na makazi ifikapo mwezi Agosti na kusisitiza kwamba zoezi la anwani za makazi ni zoezi endelevu.





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...