Na Amiri Kilagalila,Njombe
Mahakama
ya wilaya ya Makete mkoani Njombe imemsomea shtaka la ubakaji kijana
Faison Alimajani Sanga (19) mkazi wa kijiji cha Makwaranga kata ya
Ipelele anayetuhumiwa kutekeleza kosa hilo kwa mwanafunzi wa shule ya
msingi wilayani humo anayetajwa kuwa na umri wa miaka 15
Mahakama
imeeleza kuwa mtuhumiwa ametenda kosa hilo la ubakaji kinyume na
kifungu cha 130 (1) (2) e na 131 (1) ya kanuni ya adhabu sura ya 16
marejeo 2019.
Kwa upande
wa mashaidi wawili wa mashtaka akiwemo muhanga mwenyewe amesema kuwa
mnamo tarehe 12 Februari, 2022 mshtakiwa alimpeleka nyumbani kwake na
kufanya kitendo hicho huku akimuahidi ya kuwa atamuoa.
Shahidi
wa pili ambaye ni baba wa mtoto huyo amesema kuwa alipogundua binti
yake ni mjamzito na kuamua kumpeleka kwenye kituo cha afya kwa ajili ya
vipimo na ndipo alipo gundulika ni mjazito
Aidha mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo na kurejeshwa rumande mpaka tarehe 30.5.2022 kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa Tena.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...