MBUNGE wa Jimbo la Mlimba Mkoani Morogoro, Godwin Kunambi amechangia kiasi cha Sh Milioni Moja kwa ajili ya ujenzi wa Shule inayomilikiwa na Waislamu katika Halmashauri ya Mlimba huku akiahidi kuhakikisha Shule hiyo inakamilika.

Kunambi ametoa ahadi hiyo leo wakati alipoalikwa na Baraza la Waislamu (Bakwata) Halmashauri ya Mlimba katika Baraza la Eid lililofanyika katika Msikiti wa Yusuf Kata ya Mchombe.

Akizungumza katika Baraza hilo, Kunambi amesema Taasisi za Dini nchini zimekua zikichangia ukuaji wa maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo Afya, Elimu hivyo kuahidi yeye kama Mwakilishi wa wananchi kuhakikisha anatafuta marafiki zaidi watakaoichangia Shule hiyo iweze kukamilika.

" Niwasifu sana Ndugu zangu Waislamu wa Kata ya Mchombe kwa kuanzisha ujenzi wa Shule hii, Madarasa mawili mliyofikia siyo haba, kwa kuanzia natoa Sh Milioni Moja kwenye mfuko wa Taasisi na nitalibeba jambo hili kwenda kwa wadau na marafiki mbalimbali kuhakikisha linafanikiwa.

Niwaase viongozi wa Dini zote kuendelea kushirikiana na Serikali ya Rais wetu Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea maendeleo watanzania, iungeni mkono Serikali na zaidi tuzidi kumuombea Rais Samia afya njema kwani sote tunaona matunda yake kwenye uongozi wake tokea aapishwe kuwa Rais," Amesema Kunambi.

Akitoa salamu za Bakwata, Sheikh Ridhiwani amempongeza Mbunge Kunambi kwa mchango alioutoa huku akimsisitiza kuendelea kushirikiana na viongozi wa taasisi zote za Dini.







 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...