Miundombinu St Anne Marie yazidi kuwa kivutio

Na Mwandishi Wetu,  Michuzi Tv

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makala amempongeza Mbunge wa Bukoba Vijijini (CCM), Dk. Jasson Rweikiza kwa uwekezaji mkubwa alioufanya kwenye sekta ya elimu.

Alitoa pongezi hizo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam alipokuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya 14 ya kidato cha sita kwenye shule ya St Anne Marie Aacademy, iliyoko Mbezi Kimara kwa Msuguri.

 Alisema uwekezaji huo umeongeza juhudi za seerikali kuhakikisha watanzania wengi wanapata elimu na kutoa ajira kwa watanzania wengi.

“Nimeambiwa kuna walimu zaidi ya 200 hapa,  walinzi, watendaji wa mazingira, makatibu muhtasi, madereva, hili ni jambo kubwa na sisi serikali lazima tumpongeze na kumtia moyo ili aendelee kutoa huduma hii muhimu kwa watanzania,” alisema.

Pia aliwapongeza wazazi /walezi wa wanafunzi wa kidato cha sita waliohitimu kwa kutimiza wajibu wao wa kuwalea na kuwalipia ada ili wapate elimu bora katika shule bora.

Makala pia alipongeza uongozi wa shule hiyo kwa usimamizi mzuri wa shule hali ambayo imesaidia  iweze kufanya vizuri katika mitihani ya kitaifa.

“Nimesikia hapa kwenye taarifa kwamba matokeo ya darasa la nne, la saba, kidato cha pili, kidato cha nne na kitado cha sita ni mazuri sana matokeo haya mazuri yanaonesha ni kwa jinsi gani shule hii imejipanga kuhakikisha kwamba wanafunzi wote wanaohitimu hapa wanapata matokeo mazuri,” alisema

Aidha, aliwataka wamiliki wa shule nchini kutoza ada himilivu ili wazazi wengi wapate fursa ya kuwaleta watoto wao wapate elimu bora.

“Nashauri ada ya shule iwe himilivu, shule ziweke ada ambayo haiwezi kuwashinda wazazi wenye vipato vya kati kusomesha watoto wao na hiyo itatoa fursa kwa watanzania wengi kumudu kuwalipia ada watoto wao,” alisema Makala

Alisema kwa kuwa shule hiyo imezungukwa na jamii, inapaswa itoe misaada na ishiriki kwenyemaendeleo ya jamii kama vile barabara, zahanati, shule, miundombinu ya maji, ulinzi na  usafiri ili kusaidia kudumisha uhusiano chanya kati ya shule na jamii.

Alisema Serikali ya Mkoa wa Dar es salaam inatambua mchango mkubwa wa shule ya St. Anne Marie Academy pamoja na shule nyingine za binafsi na itaendelea kuweka mazingira rafiki ili kupata shule nyingi ziweze kuwekeza kwenye elimu na kutoa hudumanzuri kama za St. Anne Marie Academy.

“Naamini mafanikio haya makubwa ya shule naamini yanatokana na ushirikiano mzuri uliopo kati ya wafanyakazi wa shule hii, kujituma, kufanya kazi kwa bidii na uwekezaji mkubwa uliofanywa na uongozi wa shule hivyo naomba msirudi nyuma endeleeni kufanya kazi zenu kwa bidii ili shule hiiiendelee kupaa siku hadi siku,” alisema.

Mkurugenzi wa shule hiyo, Dk. Jasson Rweikiza alisema ataendelea kuboresha miundombinu ya shule hiyo ili kuhakikisha inaendelea kufanya vizuri kwenye mitihani yote ya ndani nay a kitaifa.

Alisema shule hiyo itamsomesha bure mwanafunzi yoyote atakayefiwa na mzazi akiwa anaendelea na masomo shuleni hapo na kwamba wapo ambao walifiwa na wazazi na hawakurudishwa nyumbani kwa kukosa ada.

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makala akimpa cheti cha kuhitimu kidato cha sita mwanafunzi Hope Shusho wa St Anne Marie Academy ya Mbezi Kimara kwa Msuguri wakati wa mahafali ya kidato cha sita mwishoni mwa wiki shuleni hapo. Anayefuata ni Mmiliki wa shule hiyo, Dk. Jasson Rweikiza na Rais wa Chama cha Wamiliki wa Shule Binafsi (TAPIE), Mahmoud Mringo
Wahitimu wa kidato cha sita wa shule ya St Anne Marie Academy wakiingia kwenye mahafali ya 14 ya shule hiyo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makala.

Mkurugenzi wa St Anne Marie Academy Dk. Jasson Rweikiza na Mkuu wa shule hiyo, Gladius Ndyetabura wakimsubiri Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makala kwenye mahafali ya 14 ya kidato cha sita yaliyofanyika shuleni hapo mwishoni mwa wiki

Wahitimu wa shule ya St Anne Marie Academy wakisoma risala yao mbele ya mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala kwenye mahafali ya 14 ya shule hiyo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo Mbezi Kimara kwa Msuguri jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...