.Mashamba yote yatakayokutwa na bangi,kutaifishwa na Serikali na kuwa mali ya Umma


Na.Vero Ignatus,Arusha


Mamlaka ya Kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa kushirikiana na Vyombo vya Ulinzi na Usalama Mkoani Arusha, imekamata kilo 220 za dawa za kulevya aina ya bangi katika matukio mawili tofauti ambapo jumla ya hekari 21 za bangi ziliteketezwa,athari katika afya na akili ya binadamu,ambapo dawa hizo zinazosumbua ni bangi na mirungi 


Akizungumza na waandishi wa habari leo 24 mei 2022 Kamishna Generali Mamlaka ya Kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevya Gerald Musabila Kusaya alieleza kuwa katika tukio la awali lililotokea tarehe 20 Mei2022 eneo la Usariver (w) Arumeru, watu 4 wanashikiliwa 2 kati yao wakiwa ni wamiliki w mashamba,na 2 wakiwa ni wafanyabiashara wa bidhaa aina ya bangi wakiyasafirisha kutoka maeneo mbalimbali ikiwemo Monduli

‘’Hali ilivyo katika maeneo mbalimbali nchini hususani mkoa wa Arusha bado tunaimani yapo mashamba ya bangi,pamoja na baadhi ya wananchi waliohifadhi magunia ya bangi,,hii ni vita kwani tunapambana na watu ambao wamejipanga kuharibu akili za watanzania na Oparesheni hii ni endelevu katika mikoa yote nchini’’ Alisema Kusaya

Aidha Kamishna Kusaya ametoa onyo kali kwa wananchi wenye tabia mbaya wanaojiingiza kwenye biashara ya kuuza dawa hizo za kulevya,aachane na biashara hiyo na kutafuta mbadala wake ambayo ni halali itakayompatia kipato,kwani Mamlaka hiyo haitawafumbia macho sheria itafuata mkondo wake.

Hata hivyo ametoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Mamlaka hiyo pamoja na viongozi wa ulinzi na usalama ili waweze kutoa taarifa ‘’Jukumu lenu ninyi wananchi tunalowaombeni tuambieni nani,yupo wapi anafanya nini suala zima juu ya dawa za kulevya na sisi kama vyombo vya ulinzi na usalama tutakachokifanya taarifa yeyote ile tutakayoipokea tutaifanyiankazi,kikamilifu ili siku ya wale wote wanaojihusisha na dawa za kulevya tuweze kuwatia mbaroni.Alisema

Amesisitiza kwa kusema kwa kuwa sheria inaruhusu katika suala zima la kutaifisha mali na vitu vingine vyote ambavyo ni zao la dawa za kulevya, kwahiyo ni vyema kulitazama kwa matazamo wa hali ya juu kwamba: Mashamba yote yatakayokutwa yakiwa yamelimwa bidhaa za bange, yatataifishwa yote yawe mali ya Serikali ili yaweze kutumiwa kwa matumizi ya umma na kupanga matumizi sahihi ya maeneo hayo.

''Tanzania tuna mazaozaidi ya 95 mbadala ambayo yanaweza kuwasababisha wananchi kuwa matajiri,mfano zao la soya linalohitajika Nchini India,mahindi ya njano yanahitajika Uarabuni ,Ufuta , kwanini usichague zao moja wapo ukajikita huko badala ya kujiingiza kwenye biashara haramu ya dawa za kulevya ambazo zinaharaibu akili na ufahamu wa vijana wetu na kuwapelekea kupata matatizo ya Akili.''alisema Kusaya''

Aidha Kusaya aliwataka wasanii wa mbalimbali nchini kutumia Sanaa zao kutoa ujumbe wenye elimu njema katika jamii na siyo ya kuhamasisha uvutaji wa bangi, kwani katika uimbaji wao au uandaaji wa muziki huwa kuna maigizo mbalimbali wanayafanya hivyo yaelekezwe katika kuelimisha jamii na siyo vinginevyo.

‘’Wasanii wetu mbalimbali wamekuwa wakifanya maigizo mbalimbali katika nyimbo zao,tunawaomba watumie vyema nafasi hiyo kwaajili ya elimu ya kuifunza jamii na isiwe vinginevyo,ikiwa kinyume tutawachukulia hatua za kisheri, Tunataka tuwe na Tanzania huru isiyokuwa na dawa za kulevya''. alisema Kusaya

Kusaya alisisitiza kuwa dawa za kulevya zinaweza kwisha pale ambapo kila Mtanzania atazichukia dawa hizo,huku akisema dawa hizo zina madhara kwa Taifa zima endapo kama biashara hiyo itakuwa inaendelea bila kutazama kwamba kuna athari gani nyuma yake.

Aidha Watuhumiwa wote wanne wameshikiliwa kutokana na tuhuma zinazowakabili na watafikishwa mahakamani mara baada ya taratibu za kisheria kukamilika.



Baadhi ya magunia yaliyokamatwa yakiwa na bidhaa za dawa za kulevya aina ya bangi yakiwa yanasafirishwa kutoka Wilaya ya Arumeru kuelekea Arusha mjini kwaajili ya kuuzwa


Moja shamba kati ya hekari 21 ambazo lilikutwa likiwa limelimwa bidhaa ya dawa ya kulevya aina ya bangi katika eneo la (w) ya Monduli


Bidhaa ya dawa ya kulevya aina ya bangi ikiteketezwa baada ya Mamlaka ya Kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa kushirikiana na Vyombo vya Ulinzi na Usalama Mkoani Arusha,kuibaini Monduli.
Kamishna Generali Mamlaka ya Kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevya Gerald Musabila Kusaya,akizungumza na waandishi wa habari katika ukimbi wa mkutano wa mkuu wa mkoa wa Arusha,ambapo aliweza kutoa ufafanuzi wa oparesheni inayoendelea juu ya kutokomeza dawa za kulevya nchini

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...